Aliyekuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya NBC ni kama anawatega Yanga hivi sasa. Nyota huyo alimaliza mkataba wak mwishoni mwa msimu na mpaka sasa hatma yake ya kusalia ama kuondoka haijajulikana. Aziz Ki aliisaidia Yanga kutwaa makombe mawili msimu uliopita likiwemo ligi ya NBC na CRDB FA CUP huku akionyesha umahili mkubwa katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika kwa kufika hatua ya robo fainali.
Aziz Ki kwa sasa amegeuka lulu kwa vilabu mbalimbali Afrika na jina lake limo katika orodha ya Mamelodi Sundowns na Orlando Pirates zote za Afrika Kusini. Nyota huyo kwa sasa thamani yake ni milioni 700 na kuna uwezekano mkubwa wa kusalia ndani ya Yanga endapo tu klabu hiyo itatimiza matakwa yake ya mkataba mpya atakaopewa lakini pia kuhitajika kwake na vilabu vyenye msuli wa fedha itawapa changamoto mpya Yanga.
Usajili wa Chama una maana yoyote kwa Yanga
Yanga wamemsajili Clatous Chama kama mchezaji huru,nyota huyu anamudu kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji sawa na Aziz Ki. Chama anauzoefu na michuano ya Afrika na amekuwa na mwendelezo mzuri kwa takribani miaka 7 akiwa na Simba miaka 6 na mwaka mmoja akiwa na RSBerkane akitwaa kombe la shirikisho Afrika na wababe hao wa Morocco.
kama Chama amesajiliwa kama mbadala wa Aziz Ki basi Yanga wamepata mbadala sahihi lakini pia kama Aziz Ki ataongeza mkataba wa kuitumikia Yanga basi eneo la ushambuliaji la Yanga litakuwa hatari sana kwa wapinzani wao.
Mikataba mipya Yasainiwa
Klabu ya Yanga imeendelea kuwaongezea mikataba baadhi ya nyota wake akiwemo Farid Musa ,Bakari Nondo Mwamnyeto na Djigui Diara ambao wote watasalia katika kikosi cha Yanga mpaka mwaka 2026. kuongezewa mikataba kwa nyota hao ni kielelezo tosha kwamba Yanga haitaki kubomoa timu yao hasa kwa wachezaji tegemezi walioisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa NBC na CRDB.
0 Comments