BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA KUWAONDOSHA NYOTA SITA KUPISHA USAJILI MPYA

 Klabu ya Yanga SC imepanga kuachana na Nyota wake 6 ambao HAWAKUWA NA NAFASI KUBWA KWENYE KIKOSI CHAO KWA MSIMU WA 2023/24. yanga wamefikia hatua za kuwaacha nyota hao ili kusajili wachezaji wengine wenye uwezo mkubwa kuelekea msimu ujao. Mpaka sasa klabu hiyo yenye makao yake jijini Dar es salaam mitaa ya Twiga na Jangwani imeshamsajili mchezaji mmoja wa kigeni ambaye ni Clatous Chota Chama kutoka Zanmbia huku ikiwapa mikataba mipya nyota wake k wa kikosi cha kwanza ambao ni Farid Musa,Djigui Diara na Bakari Nondo Mwamnyeto.

Klabu hiyo imepanga kuwapa mkono wa kwaheri wachezaji 6  ambao ni Mghana Agustine Okrah, kiungo Mahlatse Skudu Makudubela kutoka Afrika Kusini ambao msimu uliopita hawakuonyesha  kiwango kikubwa walipopata nafasi huku  Mkongo Joyce Lomalisa, Zawadi Mauya, Metacha Mnata na Joseph Guede kutoka nchini Ivory Coast mikataba yao ikifika ukomo na wao kushindwa kumshawishi mwalimu Gamondio na Benchi la ufundi.

Yanga wamejipanga kuanza kutambulisha wachezaji wake wapya waliosajiliwa msimu huu na zoezi hilo litaanza hivi klaribuni wakielekea Pre Season kwa ajili ya msimu ujao.

mpaka sasa nyota Aziz ki bado hajaweka hadharani hatma yake ndani ya Yanga baada yamkataba wake kumalizika na Yanga wanaoonekana kuhitaji huduma yake kuelekea msimu ujao.
Post a Comment

0 Comments