BETI NASI UTAJIRIKE

YANGA KUSHUSHA MASHINE NYINGINE YA KIKONGO

 Yanga bado hawajamaliza usajili. hii ni habari njema kwa mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo kuelekea msimu ujao baada ya taarifa za ndani kuvuja kuhusiana na usajili wa mshambuliaji hatari Jean Baleke. taarifa zisizo rasmi zinasema viongozi wa pande zote mbili klabu na mchezaji wameshaanza mazungumzo kuhusu mchezaji huyo.

Baleke alisajiliwa kwa mkopo na klabu ya Simba akitokea TP Mazembe na mwezi januari aliondoka klabuni hapo na kujiunga na klabu ya Al Ittihad ya Libya na baadaye alirejea tp mazembe na sasa ni mali halali ya klabu hiyo.

Safari ya Soka ya Baleke

Jean Baleke alizaliwa mwaka 2001 nchini Kongo na mwaka 2021 alijiunga na timu ya FC Aigles ya nchini humo, msimu huo huo alinunuliwa na TP Mazembe ambako alitolewa kwa mkopo kwenda Nejmeh SC. Mwezi disemba mwaka 2022 alirejea tena TP Mazembe na januari 2023 alitolewa tena kwa mkopo kwenda Simba ambako alidumu kwa mwaka mmoja na januari 2024 airejea TP Mazembe ambako alitolewa tena kwa mkopo kwenda Al Ittihad ambako mkataba wake umemalizika juni 2024 na sasa amerejea tena TP Mazembe. Kama uongozi wa pande zote mbili utakubaliana basi nyota huyo atatua jangwani kwa mkopo

Je Yanga wanauhitaji wa Mshambuliaji 

Yanga wanauhitaji wa mshambuliaji aina ya Jean Baleke kwa sababu ana uwezo mzuri wa kufunga mabao ,anauzoefu wa michuano ya kimataifa na analielewa soka la tanzania. nyota huyo mwenye miaka 21 pekee alikuwa na faida kwa klabu ya Simba kwa kipindi chote alichoitumikia klabu hiyo.Kama Baleke atatua Yanga basi ataongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga akiungana na Clement Mzize na Prince Dube.


Post a Comment

0 Comments