BETI NASI UTAJIRIKE

RONALDO ,MBAPPE ,KROOS NA GUNDOGAN VITANI LEO

 Michano ya EURO 2024 inaendelea leo hii kwa kuwakutanisha wababe wa Ulaya katika hatua ya robo fainali.Michezo hiyo inategemewa kuwa na ushindani kutokana na timu zote nne kuwa na historia ya kutwaa kombe hilo kwa miaka ya hivi karibuni lakini pia itakutanisha wachgezaji wenye majina makubwa kuanzia Cristiano Ronaldo,Kylian Mbappe,Thomas Mulller na kiungo Rodri


Mchezo wa kwanza utapigwa saa 1 jion kwa kuwakutanisha waandaaji wa michuano hiyo Ujerumani dhidi ya watoto wa mwanamfalme Hispania .Mchezo huu utakutanisha vijana wengi chipuukizi kwa pande zote mbili na unategemewa kuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na timu zote mbili kuwa na mwanzo mzuri wa mashindano kuanzia hatua za makundi mpaka mtoano.

Ujerumani

Hawa ndiyo waandaaji wa michuano hii kwa mwaka 2024. Ujerumani  walianza vyema kampeni za kusaka ubingwa kwa hatua ya makundi baada ya kupata Ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Scotland ,ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Hungary na sare ya 1-1 dhidi ya Uswizi na kuwafanya kumaliza kundi lao wakiwa na alama 7 na kufungwa mabao 2 pekee wao wakifunga mabao 8. Hatua ya 16 walikutana na Denmark na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.  Jamal Musiala ndiye atakayeongoza safu ya ushambuliaji ya Ujerumani akishirikiana na Toni Kroos ,Kai Hervat ,Gundogan na Sane.

Hispania 

Hawa wamekuwa tishio kwa hatua ya maklundi baada ya kupata ushindi katika mechi zote walizocheza.Katika hatua ya makundi Hispania ilikutana na Crotia na kushinda mabao 3-0 ,ikacheza dhidi ya Italy na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na mchezo wa mwisho wa makundi ilishinda bao 1-0 dhidi ya Albania na kuwafanya wamalize kundi wakiwa na alama 9 na mabao 5 wakiwa hawajafungwa bao lolote. Hatua za 16 bora walikutana na Georgia na kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.Morata ataiongoza safu ya ushambuliaji ya ujerumani akishirikiana na Lamine Yamal,Pedri,Rodri na Nico Williams.

Mchezo wa pili utapigwa majira ya saa 4 usiku na utawakutanisha Ureno na Ufaransa. Mchezo huu utawakutanisha wachezaji wawili muhimu katika soka la dunia,Cristiano Ronaldo anayemaliza utawala wake katika soka la dunia na Klyian Mbappe anayejenga ufalme wake mpya duniani.Mara ya mwisho timu hizo kukutana katika michuano hii ni EURO 2020 mchezo uliomalizika kwa sarte ya mabao 2-2..

Ureno

Ureno walianza vizuri hatua za makundi baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya jamhuri ya Czech kisha kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Uturuki na kupoteza 2-0 dhidi ya Georgia. katika hatua za 16 bora Ureno ilipangwa dhidi ya Slovenia mchezo uiliomalizika kwa timu zote mbili kutofungana na mchezo kuamuliwa kwa mikwaju ya penati ambapo Ureno walipata mikwaju yote ya Penati.katika mchezo huo Cristiano Ronaldo alikosa mkwaju wa Penati na mpaka sasa nyota huyo hajafunga bao lolote ndani ya dakika 90

Ufaransa

Licha ya kushamili kwa wachezaji wenye uwezo mkubwa lakini kikosi cha Didier Deschamp kilianza kampeni za kuwania ubingwa wa Euro 2024 kinyonge.katika hatua za makundi Ufaransa ilipata ushindio wa bao 1 -0 dhidi ya Austria na goli lenyewe alijifunga Maxi Welber wa Austria. Timu hiyo iliambulia sare ya 0-0 dhidi ya Uholanzi kisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Poland. hatua za 16 timu hiyo ilikutana na Ubelgiji na kuibuka na ushindi wa bao 1-0. Ufaransa wamekuwa na wakati mgumu eneo la ushambuliaji baada ya kufunga mabao 2 pekee katika mechi nne walizocheza.

Griezman na Mbappe wanakazi ya ziada hii leo kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo muhimu utakaowapeleka nusu fainali.

Post a Comment

0 Comments