Arsenal wanakaribia kufikia makubaliano ya thamani ya pauni milioni 42.1 na Bologna kwa beki wa Italia Riccardo Calafiori, 22. (Sky Sports)
West Ham wana nia ya kutaka kumnunua beki wa AC Milan mwenye umri wa miaka 26 Muingereza Fikayo Tomori. (Mail),
Aston Villa wako tayari kumuuza beki wa kulia wa Poland Matty Cash mwenye umri wa miaka 26 msimu huu mpya. (Football Insider)
Manchester United wameamua kutoanzisha chaguo la kumsajili kiungo wa kati wa Morroco Sofyan Amrabat, 27, kwa mkataba wa kudumu. (Tuttomercato - In Itali)
Klabu hiyo ya Ligi ya Premia ina nia ya kumbakisha Amrabat katika klabu hiyo baada ya muda wake wa mkopo msimu uliopita lakini wanataka kufanya mazungumzo ya mkataba mpya. (Metro)
Tottenham wanataka kumbadilisha Oliver Skipp na kiungo wa nyumbani ikiwa watamruhusu Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 23 kuondoka katika klabu hiyo. (Football Insider)
Rais wa heshima wa klabu ya Bayern Munich Uli Hoeness amependekeza beki Mholanzi Matthijs De Ligt, 24, ambaye anasakwa na Manchester United, akuondoka katika klabu hiyo msimu huu . (Sky Germany)
Kiungo wa kati wa Manchester City na Ubelgiji Kevin de Bruyne, 33, hajaafikiana makubaliano na klabu ya Saudi Arabia Al Ittihad licha ya kuwepo kwa ripoti. (Sportsport)
Paris St-Germain wako tayari kuendeleza harakati zao za kumsajili mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 25. (Fabrizio Romano)
Pamoja na Osimhen, PSG pia wanataka kuwasajili winga wa Napoli wa Georgia Khvicha Kvaratshkelia, 23, na kiungo wa kati wa Ufaransa Desire Doue mwenye umri wa miaka 19 kutoka Rennes. (Sky Sports)
0 Comments