Chelsea wako kwenye mazungumzo na Borussia Dortmund kuhusu kumnunua mshambuliaji wa Ujerumani Karim Adeyemi, 22. (Bild – in Deutsch)West Ham wanavutiwa na mshambuliaji wa Aston Villa na Colombia Jhon Duran, 20. (Sky Sports),
Manchester United wamekubaliana kwa maneno na beki wa Bayern Munich Mholanzi Matthijs de Ligt mwenye umri wa miaka 24. (Evening manchester News),Klabu ya Juventus ya Serie A bado ina nia ya kumsajili winga wa Manchester United Muingereza Jadon Sancho, 24. (Sky Sports),
Nottingham Forest na Wolves wanavutiwa na mlinzi wa Le Havre Mfaransa Etienne Youte Kinkoue, 22. (Football Insider),Baadhi ya mashabiki wa Marseille wameitaka klabu hiyo kusitisha hamu yake ya kumnunua mshambuliaji wa Manchester United Muingereza Mason Greenwood, 22. (Mirror).
Manchester United ina makubaliano kimsingi ya kumsajili beki wa Ufaransa Leny Yoro, 18 kutoka Lille. (Sky Sports),Lakini Real Madrid pia bado wana nia ya kutaka kumnunua Yoro licha ya msimamo wa klabu hiyo ya Premier League. (Fabrizio Romano),
0 Comments