Manchester United ilifikiria kupata kitita kikubwa kutokana na mauzo ya nahodha Bruno Fernandes, 29, lakini kiungo huyo wa kati wa Ureno anatarajiwa kusalia katika klabu hiyo na kusaini mkataba mpya. (Mirror)
Ofa ya Arsenal ya euro milioni 47 ya kumnunua Riccardo Calafiori imekataliwa na klabu ya Bologna ambayo inataka angalau euro milioni 50 kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia. Chelsea pia wanavutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)
Mchezaji huru Dele Alli ameonekana akifanya mazoezi kwa bidii huku akitafuta klabu mpya baada ya kuondoka Everton mkataba wake ulipokamilika mwishoni mwa msimu uliopita. (Express)
Beki wa Ufaransa William Saliba anaweza kuondoka Arsenal msimu huu huku Real Madrid wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Mirror)
Mshambuliaji wa Napoli Victor Osimhen, 25, anatarajiwa kuwa sehemu ya maandalizi ya klabu yake kwa msimu ujao wiki ijayo huku Manchester United, Chelsea na Arsenal zikiwa na nia ya kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria. (Football Italia)
West Ham wanafikiria kuwasilisha ofa mpya kwa mlinzi wa Nice Jean-Clair Todibo baada ya ofa ya pauni milioni 24.5 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kukataliwa. (Mail)
Post a Comment
0
Comments
MERIDIAN BET
EURO 2024
Kuanzia tarehe 14 june to 14 july AMOSPOTIXTRA TEAM itakuwa ujerumani kukuletea michuano ya EURO2024
0 Comments