BETI NASI UTAJIRIKE

SOUTHGATE AMEWEKA REHANI KIBARUA CHAKE DHIDI YA UHOLANZI

 Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate leo hii anakibarua kigumu kuhakikisha timu hiyo inafuzu hatua ya fainali dhidi ya Uholanzi.Kocha huyo alikabidhiwa mikoba ya kuinoa Uingereza mwaka 2016 na amefanikiwa kuiongoza timu hiyo katika michuano mbalimbali ikiwamo Kombe la dunia mwaka 2018 na 2022, kombe la Euro mwaka 2018,2020 na sasa 2024 pamoja na kombe la Uefa national league.


Mafanikio makubwa aliyoyapata ni kufika fainali za michuano ya Euro 2020 akiukosa ubingwa mbele ya Italy kwa mikwaju ya penati.Southgate amekuwa kocha mwenye kurudisha matumaini kwa Waingereza kwaa kujenga timu yenye ushindani kila anaposhiriki katika michuano.

Msimu huu kocha huyo ameiongoza Uingereza katika michezo 3 ya makundi akishinda mchezo mmoja na sar michezo miwili. kocha huyo alifanikiwa kuwatoa Slovakia kwa ushindi wa mabao 2-1 katika hatua za 16 bora na kuwaondosha Uswizi kwa mikwaju ya Penati 5-3. 

Usiku wa leo Uingereza itavaana na Uholanzi katika hatua ya nusu fainali kumtafuta mshindi wa kucheza fainali dhidi ya Hispania siku ya jumapili tarehe 14. Kwa upande wa Uholanzi wao wamefanikiwa kufika hatua ya nusu fainali baada ya kushinda michezo ya robo fainali dhidi ya Uturuki na hatua ya 16 bora dhidi ya Romania. kwa upande wa makundi timu hiyo ilifanikiwa kushinda michezo dhidi ya Poland na Iceland ikitoa sare dhidi ya Ufaransa.

Mpaka sasa Southgate anaamini uwezo kwa wachezaji wake wa kikosi cha kwanza ambao Pickford,Kyler Walker ,Johnston,Konsa,Bukayo saka,Maino,Rice,Trippier,Jude Bellingham,Phil Foden na Harry Kane. klocha huyo amekuwa akitumia mfumo wa 3-4-3.Kocha huyo amebadili kikosi chake kwa msimu huu baada ya kutowajumuisha Marcos Rashford ,Harry Maguire,Luke,Jodan Sancho ,Jammie Vardy

Kama kocha huyo atapoteza katika mchezo huo basi kibarua chake kitakuwa shakani na kama Uingereza itafuzu fainali na kutwaa ubingwa mbele ya Hispania basi kocha huyo atakuwa ameonda ukata wa makombe kwa nchi hiyo na jinal ake litaheshimika katika soka la nchi hiyo ambayo mara ya mwisho kutwaa ubingwa ni mwaka 1966 wakitwaa kombe la dunia.

Kocha huyo amebadili kikosi chake kwa msimu huu baada ya kutowajumuisha Marcos Rashford ,Harry Maguire,Luke Show ,Jodan Sancho kutoka Manchester United.

Post a Comment

0 Comments