Ratiba ya michuano ya CAF ikijumuisha kombe la shirikisho na ligi ya mabingwa ulaya imekwishatangazwa na Tanzania bara itapeleka timu 4 ambazo ni Yanga na Azam ligi ya mabingwa Africa ,Coastal Union na Simba wao watashiriki michuano ya kombe la shirikisho.
Klabu za Coastal Union,Azam na Yanga zitaanzia hatua za awali katika michuano wanayoshiriki huku simba ikianzia raundi ya kwanza kuweza kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho. Simba imepata nafasi ya kuanzia raundi ya kwanza baada ya kujikusanyia alama 39 za CAF na ni moja ya timu nane bora za Africa zitakazoanzia hatua ya kwanza ya michuano hiyo.
Mpangilio wa ratiba
Azam FC
Azam FC imepangwa na klabu ya APR Rwanda na mchezo wa kwanza utapigwa Agosti 16 na 18 jijjini Dar es salaam, raundi ya pili mchezo itapigwa nchini Rwanda kigali kati ya Agosti 23 na 25.kama timu hiyo itasonga mbele basi itakutana na mshindi kati ya Pyramids ya Misri au JKU ya Zanzibar na kama watashinda mchezo huo basi wataingia moja kwa moja hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Africa.
Young Africans
Klabu ya Yanga imepangwa kucheza na Vitalo FC ya nchini Burundi .Mchezo wa kwanza utachezwa Agosti 16 na 18 jijini Bujumbura nchini Burundi na mchezo wa marudiano utapigwa jijini Dar es salaam kati ya tare 23 na 25 .Kama Yanga ataibuka na ushindi katika mchezo huo atakutana na .... na kama atashinda mchezo huo basi atakwenda hatua za makundi za michuano ya ligi ya mabingwa Africa.
Coastal Union
Klabu hiyo yenye makazi yake jijini Tanga itaanza kampeni za kufuzu hatua za makundi za kombe la shirikisho dhdi ya FC Bravo ya Angola na kama itashinda mchezo huo itavaana na FC lupopo ya nchini Kongo ili iweze kufuzu hatua za makundi za michuano hiyo.Coastal Union wanaonekana kujiandaa vyema katika michuano hiyo kwa kufanya sajili za nyota wenye uzoefu.
Simba
Simba wataanzia raundi ya pili ya michuano ya kombe la shirikisho ili iweze kufuzu hatua za makundi. Timu hiyo itasubiri mshindi kati ya Uhamiaji Zanzibar na Libya 1 inayoshiriki ligi kuu nchini Libya.
0 Comments