BETI NASI UTAJIRIKE

SIMBA YAZALIWA UPYA KUELEKEA MSIMU WA 2024/25

 Kuelekea msimu wa 2024/25 Klabu ya Simba SC imeonyesha nia ya kufanya vizuri katika michuano ya NBC Premier League,CRDB FA CUP na Kombe la shirikisho la CAF. Simba ilimaliza msimamo wa ligi ya NBC ikishika nafasi ya tatu nyuma ya Azam na Yanga,Iliondoshwa katika hatua ya robo fainali katika makombe ya FA na Ligi ya mabingwa Afrika hivyo kuwalazimu kufanya mabadiliko makubwa ndani ya kikosi kwa msimu utakaoanza Agosti 2024.


Mpaka sasa klabu hiyo imeachana na waliokuwa nyota wa kikosi hicho akiwemo kapteni John Raphael Bocco ambaye amestaafu na sasa amekuwa kocha wa timu ya vijana. wachezaji mahili wa kigeni katika safu ya ushambuliaji ambao ni Cloutas Chota Chama,Saido Ntibazonkiza na Luis Miquissone. Simba hawakuishia hapo waliamua kumwacha beki mkongwe Kenedy Juma,Shaban Chilunda na Hennock Inonga

Ukitazama orodha ya wachezaji walioachwa unaweza kujiuliza je simba imekusudia nini kuelekea msimu ujao? jibu ni rahisi tu Simba inakusudia kuzaliwa upya katika kila safu ya kiwanja. imekusudia kufanya vyema kwa msimu ujao na mpaka sasa imeonyesha ni namna gani wamejipanga kwa msimu huo. Mpaka sasa Simba imewabakiza baadhi ya nyota waliokuwa ndani ya kikosi chao kwa kuwaongezea mikataba akiwemo Kibu Denis,Mzamiru Yasin na Israel Mwenda.

Mbali na kuwaongeza mikataba nyota hao lakini pia imewasajili nyota mbalimbali .Hii ni orodha ya baadhi ya nyota hao waliosajiliwa mpaka sasa 

1.Lameck Lawi - Beki

Kijana Lameck Lawi kutoka Coastal Union ya Tanga ndiye aliyekuwa wa kwanza kusajiliwa ndani ya kikosi cha Simba.Lawi ni beki wa kati na msimu wa 2022/23 alifanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji chipukizi. kwa msimu wa 2023/24 nyota huyo alifanikiwa kuisadia Coastal Union kumaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ya NBC na kuipeleka timu hiyo katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika lakini pia aliisaidia timu hiyo kufika hatua ya nusu fainali ya kombe la CRDB FA. lAWI anacheza nafasi ya beki wa kati na pembeni,usajili wake utamfanya aingie moja kwa moja  kikosi cha kwanza baada ya Inonga na kenedy juma kuondoshwa kikosini hapo.

2.Joshua Mutale- Winga na Mshambuliaji

Nyota huyu wa kizambia ametoka Power Dynamo na anasifa ya kucheza maeneo matatu ya uwanja .anaweza kucheza kama winga wa kulia au kushoto lakini pia anaweza kucheza kama mshambuiliaji wa kati.Nyota huyu anaumri wa miaka 22 na atasalia ndani ya Simba mpaka mwaka 2027.

3.Steven Mukwala Mshambuliaji wa kati

Nyota huyu amesajiliwa kuja kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji ndani ya Simba . mwanzoni mwa msimu wa 2023/24 Simba ilikuwa na washambuliaji watatu ambao ni Jean Baleke ,John Boko na Moses Phiri baadaye nyota hao waliondoshwa kikosini kwa sababu mbalimbali hivyo majira ya dirisha dogo yaliwalazimu simba kuingia tena sokoni kumsajili mshambuliaji wa kati ambaye ni Fred . kusajiliwa kwa Mukwala kutakwenda kuiimalisha safu ya ushambuliaji ya Simba kwani yota huyo mwenye miaka 24 anauzoefu na soka la Afrika baada ya kuvitumikia vilabu vya Maroons ,Vipers,URA  na Asante Kotoko ya Ghana 

4.Ahoua Jean Charles Kiungo mshambuliaji

Ahoua ni kiungo mshambuliaji na amesajiliwa kama mbadala wa chama na Saido Ntibazonkiza .Nyota huyu anacheza katika nafasi tatu uwanjani na anategemewa kuwa mbadala sahihi wa nyota hao.Ahoua anacheza eneo la kiungo mshambuliaji lakini pia anamudu nafasi za winga wa kulia na kushoto.nyota huyu mwenye miaka 22 pekee amefanikiwa kuchezea klabu za LYS Sanddra,Sewe Sports na Stella Club zote za Ivory Coast

Post a Comment

0 Comments