BETI NASI UTAJIRIKE

SIMBA NOMA YAWEKA NA KUVUNJA REKODI ZAKE

 Zikiwa zimesalia siku tatu kufikia kilele cha Simba Day klabu hiyo imeandika historia mpya kwa kumaliza mauzo ya tiketi zote elfu 60 za tamasha hilo . Simba wamevunja rekodi yao wenyewe waliyoiweka mwaka 2023 ya kumaliza mauzo ya tiketi zote siku mbili kabla ya Simba day.

Kauli mbiu ya UBAYA UBWELA imezaa matunda kwa timu hiyo na kuwapiku wapinzani wao Yanga ambao watahitimisha kilele cha wiki ya wananchi tarehe 04 agosti siku moja baada ya ile ya Simba Day. Mkurugenzi mtendaji bwana Imani kajula amenukuliwa akisema

 " Simba tumeonyesha ukubwa wetu na tumeweza kuvunja rekodi yetu ya mwaka jana ambapo tuliuza tiketi zote siku mbili kabla ya simbaday ,mwaka huu tumeuza tiket zote siku tatu kabla ya Simba Day "

"Hongereni sana mashabiki wetu tukutane uwanja wa mkapa kwenye SimbaDay ya Ubaya Ubwela .Timu yeyote kubwa inapimwa na ukubwa wa sapoti ya mashabiki wake ,na hii inadhiuhirisha kwanini mashabiki wa Simba mlichaguliwa kuwa mashabbiki bora barani Afrika"





Post a Comment

0 Comments