BETI NASI UTAJIRIKE

RED ARROWS MABINGWA WAPYA CECAFA

 Michuano ya DAR PORT CECAFA imetamatika jioni hii kwa timu ya Re Arrows ya nchini Zambia kutwaa ubingwa baada ya kuifunga APR ya rwanda kwa mikwaju ya penati 10-9 mchezo uliopigwa Dimba la KMC jijini Dar es salaam.



Rick Banda wa Red Arrows alikuwa wa kwanza kufunga bao la kuongoza dakika ya 69 lakini Mamadou wa APR alisawazisha bao hilo dakika ya 90+1 na mchezo huo kumalizika kwa sare ya mabao 1-1 ndipo refarii Arajiga aliamulu timu hizo kwenda dakika 120 zilizomalizika kwa timu hizo kutofungana.

Mwamuzi aliamuru timu hizo kupiga penati 5 kwa kila timu na zote zilifungwa ,kama haitoshi mwamuzi huyo aliongeza penati nyingine ndipo RED ARROWS walifanikiwa kupata penati zote 10 na APR walikosa penati ya mwisho kwa kupaisha.

Red Arrows inakuwa klabu ya kwanza nje ya Afrika Mashariki kutwaa kombe hilo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1967 na imefanikiwa kuondoka na kitita cha dola 30000.

kipa wa APR Pavel Ndzila alichaguliwa kuwa kipa bora wa michuano  hiyo huku Mohammed Abdelrahmana akiwa mfungaji bora wa michuano kwa mabao matano na Clement Niyigena alikuwa mchezaji bora wa mashindano. Nyota hao walivuna kiasi cha dola 2000 kila mmoja.

Michuano hiyo ilianza julai 9 ikishirikisha timu 12 ,Wenyeji wakiwa ni Singida Fountain Gate ,Coastal union na JKU ambazo zote zilishindwa kufuzu hatua ya nusu fainali na kuwaruhusu wageni kutawala michuano hiyo iliyotamatika . Klabu ya APR imefika fainali ya michuano hiyo mara tisa ikifanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo mara 3 mwaka 2004,2007 na 2010

Post a Comment

0 Comments