BETI NASI UTAJIRIKE

MIQUISSONE AREJEA NYUMBANI BAADA YA KUACHANA NA SIMBA

 Klabu ya UDSongo imemtambulisha rasmi aliyekuwa mchezaji wa Simba Luis Jose Miquissone.Nyota huyo aliyerejea Simba mwanzoni mwa Msimu wa 2023/24 akitokea Al Ahly ya Misri hakuwa na kiwango kizuri ndani ya klabu hiyo na mwishoni mwa msimu huo alipewa mkono wa kwa heri


Miquissoni amerejea UD Songo ya nchini Msumbiji baada ya kuondoka kwa miaka minne. Nyota hiuyo  alianza  soka na kucheza kwa mafanikio Miquissone alishinda Kombe la Msumbiji mnamo 2016 na ubingwa wa kitaifa mnamo 2017.

msimu wa 2019 akiwa na klabu hiyo alisajiliwa na  Simba mwaka 2020 na kufanya vizuri akiisaidia klabu hiyo kufika robo fainali ya mabingwa Afrika na kutwaa ubingwa wa ligi kuu na FA kisha kwenda kwa mabingwa wa Afrika Al Ahly.

Akiwa Al Ahly alikuwa chaguo la kwanza la kocha Pitso Mosimane ,kutimuliwa kwa kocha huyo kulimfanya kukosa nafasi ya kudumu ndani ya kikosi cha Al Ahly na na baadaye kupelekwa ALAbbhaya SaudiArabia na mwaka 2023 aliuzwa kurudi Simba 

Post a Comment

0 Comments