BETI NASI UTAJIRIKE

MESSI AIPELEKA ARGENTINA FAINALI COPA AMERIKA

 Mshambuliaji Lionel Messi amefanikiwa kufunga bao lake la kwanza la michuano ya COPA AMERIKA 2024 na kuisaidia timu yake Argentina  kufika fainali wakiilaza Canada kwa mabao 2-1. Katika mchezo huo kocha Nicolas Scaloni hakufanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chake kwa kuwaanzisha emiliano Martinez,Montiel,Cristiano Romelo,Lisandro Martinez,Taglifiaco,Di Maria ,de paul,Enzo Fernandez.MaxcAllister,Julian Alkvarez na Lionel Messi.

Julian Alvarez alikuwa wa kwanza kuipa Argentina bao la uongozi dakika ya 21 akipokea pasi kutoka kwa De Paul na bao la pili lilifungwa na Lionel Messi dakika ya 51 akipokea pasi kutoka kwa Enzo Fernandez.

kwa miaka minne mfululizo Argentina imekuwa na kiwango cha hali ya juu baada ya kutwaa ubingwa wa Copa America mwaka 2021 kwa kuiadhibu brazil bao 1-0 katika dimba la Maracana nchini Brazil ,mwaka huo pia timu hiyo ilishiriki michuano ya Finalisma na kuibuka na ushindi mbele ya Italy.mwaka 2022 timu hiyo ilifanikiwa kutwaa taji lake la tatu la kombe la dunia baada ya kuitandika Ufaransa katika michuano hiyo iliyofanyika nchini Qatar.

Mafanikio haya yanamfanya kocha Nicolas Scaloni kuwa na rekodi za kipekee katika soka la Argenntina kwa miaka ya hivi karibuni sawa na kapteni wake Lionel Messi .

Argentina wanafuzu hatua ya fainali ya COPA AMERICA kwa mara ya pili mfululizo wakifanya hivyo mwaka 2021 na kutwaa kombe hilo lakini pia rekodi za Argentina katika michuano hiyo ni nzuri baaada ya kutwaa kombe hilo mara 15 tangu  kuanzishwa kwake. 

Fainali ya michuano hiyo itapigwa usiku wa tarehe 15/7 majira ya saa 9 alfajiri kati ya Argentina vs Uruguay/Colombia


Post a Comment

0 Comments