BETI NASI UTAJIRIKE

MANARA AFUNGULIWA RASMI NA TFF

AAliykuwa afisa habari wa Yanga Haji Manara amemaliza rasmi adhabu ya kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miaka miwili hukumu iliyotolewa Julai 21 mwaka 2022 na kamati ya maadili ya TFF.

Manara alifungiwa na kamati ya maadili baada ya kurusha maneno makali kwa raisi wa TFF  Bw.Wales Karia wakati wa mchezo wa fainali kati ya Yanga na Azam jijini Arusha. Katika mchezo huo Manara alionekana akizoizana na raisi huyo wa TFF na alinukuliwa akisema  " Wewe unanifatafata sana ,hii ni mara ya tatu ,sikuogopi kwa lolote ,kwa chochote na huna cha kunifanya" Kwa mujibu wa kamati ya maadili Manara alikutwa na hatia ya kuvunja kifungu cha 73 ibara ya 5 ya mwaka 2021inayohusu mienendo ya tabia na maadili.

Mbali na hukumu ya miaka 2 ya kutojihusisha na soka manara alipigwa faini ya shilingi milioni 20.Hii leo tarehe 22 Julai 2024 manara amekamilisha kifungo chake cha miaka miwili na atarejea kwenye majukumu yake ya kiutendaji ndani ya Yanga

Post a Comment

0 Comments