BETI NASI UTAJIRIKE

KANE NA BELLINGHAM WAIPELEKA UINGEREZA ROBO FAINALI EURO

 Timu ya taifa ya Uingereza imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali michuano ya EURO 2024 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Slovakia. Schranz kutka Slovakia ndiye aliyekuwa wa kwanza kufunda bao dakika ya 25 na Shukrani za kipekee zimwendee nyota wa Real Madrid na Uingereza Jude Bellingham aliyesawazisha bao hilo dakika ya 90+5 na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya mabao 1-1 dakika 90 na kupelekea mchezo huo kuongezwa dakika 30 ili kumpata mshindi atakayefuzu hatua ya robo fainali


 Mshambuliaji wa Bayern Munich na Uingereza Harry Kane alifanikiwa kuandika bao la pili katika dakika ya 91 na kuifanya Uingereza kuingia robo fainali kwa ushindi wa mabao 2-1..Mpaka sasa timu ya Uingereza imecheza jumla ya  michezo minne ya Uero na kupata ushindi wa michezo 2 dhidi ya Slovakia (hatua ya 16 bora) na Serbia huku ikipata sare dhidi ya Denmark na Slovenia hatua ya makundi. Timu hiyo ilimaliza kundi ikiwa na alama tano.

Uingereza imeungana na mataifa ya Hispania ,Ujerumani,na Uswizi na katika hatua hiyo ya robo fainali Uingereza itavaana na Switzerland mchezo utakaopigwa Julai 6.

Post a Comment

0 Comments