Timu ya taifa ya Hispania imeendeleza ubabe baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Georgia mchezo wa hatua ya 16 bora michuano ya Euro 2024 . Kwa matokeo hayo Hispania imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali na itavaana na mwenyeji wa mashindano hayo Ujerumani tarehe 5 Julai.
Felippe Ruiz aliipa Hispania bao la pili baada ya kupokea pasi kutoka kwa Lamine Yamal,Wiliam alifunga bao la 3 dakika ya 75 huku Olmo akihitimisha ushindi wa mabao 4 kwa kumalizia pasi iliyotoka kwa Oyarzabal dakika ya 83.
Hispania imecheza michezo mitatu katika hatua ya makundi ya michuano hiyo na kuvuna alama 9 kwa kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Crotia, ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Italy ,ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Albania na hatua ya mtoano imeshinda 4-1 dhidi ya Georgia.
Kiufundi timu ya hispania inamwenendo mzuri kwa kushinda mechi zote 4 na kufunga mabao 9 huku ikifungwa bao 1 tu.Ushindi huu wa Hispania unaifanya timu hiyo kuungana na Uswizi,Ujerumani,Uingereza katika hatua za robo fainali.
0 Comments