BETI NASI UTAJIRIKE

HISPANIA YATINGA FAINALI ZA EURO 2024

 Timu ya taifa ya Hispania imefanikiwa kutinga fainali za michuano ya EURO 2024 inayoendelea nchini Ujerumani. Hispania imefikia hatua hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ufaransa . Hii inakuwa fainali ya kwanza kwa timu hiyo toka mwaka 2012 walipotwaa ubingwa wa michuano hiyo kwa kuiadhibu Italy mabao 4-0.


Tathmini ya mchezo

Kikosi cha Ufaransa kiliundwa na Mike Maigan,Joles Kounde,Dayot Upamekano,William Saliba ,Theo Hernandez,Ngolo Kante,Tchouameni,Adrian Rabiot,Dembele,Kolo Muani na Kyliani Mbappe.

Kikosi cha Hispania kiliundwa na Unai Simon,Jesus Navas,Nacho,Laporte ,Marc Cucurela,Rodri,Fabian Ruiz,Lamine Yamal,Dani Olmo ,Nicco Williams na Alvaro Morata.

katika mchezo huo mshambuliaji wa Ufaransa Kolo Muani alikuwa wa kwanza kupachika bao dakika ya 9 akipokea pasi kutoka kwa Kylian Mbappe. Dakika ya 21 kinda anayechipukia kutoka hispania Lamine Yamal alisawazisha bao hilo na dakika ya 25 Dani Olmo alifanikiwa kupachika bao la pili na mchezo kumalizika kwa hispania kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Msimu huu wa mashindano umekuwa bora zaidi kwa Hispania baada ya kushinda mechi zote 6  ndani ya dakika 90 wakifunga jumla ya mabao 13 na kufungwa mabao 3 pekee huku golikipa Unai Simon akiwa na clean sheet 3.

Hispania inamsubiri mshindi kati ya Uingereza na Uholanzi katika hatua ya fainali itakayopigwa siku ya jumapili tarehe 14.Kocha Luis De La Fuente anaweza kuingia katika historia ya hispania kama ataibuka na ubingwa wa Euro 
Post a Comment

0 Comments