Safari ya kufika robo fainali
Argentina
Timu ya taifa ya Argentina imefika hatua za robo fainali baada ya kuvuna alama 9 katika kundi A. Kundi hilo lilikuwa na timu za Canada,Peru na Chile.Ubora wa kikosi cha Argentina ikiongozwa na Laurato Martinez uliisaidia timu hiyo kuwa kinara wa kundi hilo.
Equador
Timu ya taifa ya Equador ilimaliza hatua za makundi kwa kushika nafasi 2 ikiwa na alama 4 katika kundi b lililokuwa na timu za Jamaica,Mexico na Venezuela. Equador walishinda mchezo mmoja dhidi ya Jamaica na wakapata sare ya bila kufungana dhi ya Venezuela na kupoteza mbele ya Mexico.
Je Messi atang'aa katika mchezo huo?
Kwa mara ya kwanza messi ameshindwa kufunga bao lolote katika michezo miwili aliyocheza hatua ya makundi. Messi alicheza michezo dhidi ya Chile na Canada na alilazimika kukaa nje kwenye mchezo wa mwisho wa kundi dhidi ya Peru baada ya kupata maumivu ya nyama za paja.
Nyota huyo anategemewa kurejea leo kwenye mchezo dhidi ya Equador na wengi wanaamini haya ni mashindano ya mwisho ya nyota huyo kuitumikia Argentina.
Messi akiwa na Argentina amefanikiwa kutwaa makombe mawili makubwa likiwemo Copa America kwa mwaka 2020 na kombe la dunia mwaka 2022 pale nchini Qatar. kwa sasa anaitumikia klabu ya Inter Miami ya nchini marekani mahala ambapo Copa America inachezwa.
0 Comments