BETI NASI UTAJIRIKE

HATMA YA JOSHUA KIMMICH IPO SHAKANI BAYERN MUNICH

Joshua Kimich amebakiza miezi 12 tu kumaliza mkataba wake ndani ya Bayern Munich. Nyota huyo alijiunga na Bayern Munich mwaka 2015 akitokea VFB stuttgart na ameisaidia klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Bundesliga mara 8, na Ubingwa UEFA mara moja.



 Msimu wa 2023/24 ulikuwa mgumu kwa nyota huyo chini ya Thomas Tuchell na uongozi wa klabu hiyo unapata kigugumizi kuanza mazungumzo ya kumuongezea mkataba chini ya kocha mpya Vicente Kompany.

Vilabu vya Barcelona,Manchester United na Real Madrid vimeonekana kuhitaji huduma ya nyota  huyo mwenye miaka 29.Mkurugenzi wa ufundi wa Bayern Munich amenukuliwa akisema kila mchezaji ndani ya Bayern Munich anapaswa kuonyesha uwezo wake wote ili kusalia ndani ya kikosi hicho.

Joshua Kimmich amekwishacheza michezo 505 mpaka sasa akifunga mabao 54 na kutengeneza mengine 120 amekuwa akicheza katika nafasi tatu uwanjani akicheza kama kiungo mshambuliaji,kiungo wa ulinzi na mlinzi wa kulia.


 



Post a Comment

0 Comments