BETI NASI UTAJIRIKE

BARBARA GONZALEZ KUREJEA SIMBA BAADA YA KAJULA KUJIUZULU

 Mashabiki wa Simba wameonyesha nia ya kumtaka aliyekuwa CEO wa klabu hiyo Babra Gonzalez kurejeshwa nafasi ya CEO itakayokuwa wazi kuanzia Septemba 1 baada ya CEO wa klabu hiyo Imani Kajula kutangaza rasmi kustaafu tarehe 31 Agosti 2024.

Wadau wa klabu hiyo wanaamini mwanadada huyo anauwezo mkubwa wa kiutendaji baada ya kufanya hivyo toka mwaka 2021 alipoteuliwa na raisi wa heshima Mohammed Dewji  mpaka alipojiuzulu Disemba 10 mwaka 2022. Barbara anakumbukwa kwa namna alivyoongeza thamani kwa klabu ya simba ikiwemo kusaini mkataba wa udhamini na kampuni ya M BET wenye  thamani ya bilioni 25 

Barbara anakumbukwa kwa namna alivyoimarisha idara ya habari na mawasiliano,kurejesha nidhamu kwa wachezaji na kuimarisha idara ya menejimenti. Chini ya Babra Simba ilifanikiwa kusaini mikataba ya matengenezo na usambazaji wa jezi za Simba tenda ambayo alishinda Fred Vunjabei na mkataba ule uliipa Simba kiasi cha bilioni 3 na kubwa kabisa ni ujenzi wa uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo wa Mo sports Arena.

hapo jana klabu hiyo ilitoa barua inayoonyesha kupokea na kuridhishwa na maamuzi ya mtendaji huyo mkuu



Post a Comment

0 Comments