Timu ya taifa ya Argentina imefuzu hatua ya nusu fainali COPA AMERICA 2024 baada ya kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penati dhidi ya Equador. Katika mchezo Laurato Martinezz alikuwa wa kwanza kuipatia Argentina bao la kwanza dakika ya 35 na mchezo huo kwenda mapumziko kwa Argentina kuwa mbele kwa bao (1-0).
Dakika ya 62 Mshambuliaji wa Equador Enner Valencia alikosa mkwaju wa penati lakini Kelvin Rodriguez alisawazisha bao hilo dakika ya 90+1 na kuufanya mchezo huop kumalizika kwa sare ya mabao (1-1) na kuzitaka timu hizo kwenda katika mikwaju ya penati kuamua timu ya kufuzu nusu fainali.
Lionel Messi aliyerejea kwenye kikosi cha Argentina baada ya kukosekana kwenye mchezo dhidi ya Peru alikuwa wa kwanza kupiga penati na kwa bahati mbaya aliikosa penati hiyo. Julian Alvarez,Mac allister,Montril na Otamendi kwa upande wa Argentina walipiga penati zao kwa ustadi mkubwa na kuwafanya Agentina kuibuka na ushindi wa mabao 4-2.
Argentina imefanikiwa kuwa timu ya kwanza kutinga nusu fainali na sasa itasubiri michezo ya jumamosi na jumapili kujua hatma yake katika michuano hiyo.
Laurato Martinez ameendelea kuwa kipongozi wa mabao akifunga mabao 4 katika mechi nne alizocheza za michuano hiyo akifuatiwa na Vinicius Junior mwenye mabao 2 katika michezo 3 sawa na Maximilian Araujo na Darwin Nunez wote wa Uruguay,Salomon Rondon na Bello wote wa Venezuela.
Michuano hiyo itaendelea siku ya jumamosi na jumapili kwa kuzikutanisha timu za Venezuela vs Canada kisha Colombia vs Panama na Brazil vs Uruguay
0 Comments