Timu ya taifa ya Argentina imefanikiwa kutwaa ubingwa wa copa america kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Colombia.shukran za kipekee zimwendee mshambuliaji Laurato Martinez aliyefunga bao hilo dakika ya 112 ya mchezo.
Katika mchezo huo mgumu mchezaji bora wa muda wote lionel Messi alitolewa nje ya uwanja dakika ya 64 baada kuumia kifundo cha mguu wa kulia. Messi hakuwa katika kiwango kizuri msimu huu wa mashindano akifunga bao moja pekee.
Mshambuliaji Laurato Martinez ndiye kinara wa ufungaji mabao wa michuano hiyo akifunga mabao matano likiwemo la fainali . Mshambuliaji mwingine wa Argentina ni Julian Alvarez mwenye mabao 3 .
Argentina imetwaa kombe la nne ndani ya miaka mitatu ikishinda makombe ya copa America mara mbili mfululizo mwaka 2021 na 2024 ,kombe la finalisma dhidi ya italy na kombe la dunia mwaka 2022 dhidi ya Ufaransa nchini Qatar.
Lionel Messi anazidi kumpiku mpinzani wake Cristiano Ronaldo kwa idadi ya mafanikio kwa timu za taifa akiiwezesha Argentina kutwaa makombe makubwa manne na Cristiano Ronaldo kutwaa makombe mawili pekee kwa timu ya taifa
0 Comments