BETI NASI UTAJIRIKE

TIMU ZILIZOFUZU 16 BORA EURO 2024 UJERUMANI

 Michuano ya Euro 2024 inayoendelea nchini Ujerumani imeendelea kuwa gumzo kutokana na ushindani mkubwa unaoonyeshwa na timu shiriki. Michuan hiyo imemalizika kwa raundi ya pili ya hatua ya makundi na inaendelea leo hii kwa raundi ya tatu na ya mwisho kuelekea hatua ya 16 bora.


Baadhi ya timu zimekwisha fanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora baada ya kupata alama 6 katika mechi mbili walizocheza huku timu nyingine zikipambana walau kupata nafasi ya tatu kuweza kucheza hatua ya 16 bora kama best looser.

Timu ya taifa ya ujerumani imefanikiwa kushinda michezo dhidi ya Scotland na Hungary na kuvuna alama 6 na kuifanya timu hiyo kuongoza kundi A wakifuzu moja kwa moja hatua ya 16 bora.

Timu ya taifa ya Hispania imefanikiwa kufika hatua ya 16 baada ya kupata ushindi dhidi ya Crotia na Italy na imefanikiwa kujikusanyia alama 6.

Timu ya taifa Ureno imefanikiwa kuingia hatua ya 16 baada ya kupata alama 6 wakipata ushindi katika mechi dhidi ya Czech Republic na Turkey.

Ugumu wa kundi E

Kundi E ndilo kundi lenye ushindani mkubwa kwa raundi zote mbili.kundi hili linaundwa na Romania,Belgium,Slovakia na Ukraine. kila timu ina alama 3 ikiwa na maana kila timu ilipata ushindi wa mechi 1 na kupoteza mechi 1 kati ya mechi 2 iliyocheza.kundi hili litaamuliwa katika raundi ya tatu kwa timu mbili kwenda hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

wakali wa Play OFF

Timu inayoshikilia nafasi ya 3 katika kila kundi inaweza kucheza michezo ya mtoano hatua ya 16 bora endapo tu itafanikiwa kumaliza hatua ya makundi ikiwa na alama nyingi pamoja na magoli mengi ya kufunga. mpaka sasa timu za Austria,Slovakia,Albania na Slovenia zipo katika nafasi nzuri ya kucheza hatua hizo lakini kama hazitapata matokeo mazuri basi timu za Czech Republic na Scotland zinaweza kujipambanua na kucheza hatua ya mtoano.

Post a Comment

0 Comments