BETI NASI UTAJIRIKE

SABABU ZA KUTOFANYIKA PAMBANO LA MWAKINYO ZAELEZWA

 Bondia Hassan Mwakinyo ameshindwa kupanda ulingoni dhidi ya Patrick Allotey wa Ghana baada ya mwakilishi wa WBO Afrika kutofika ukumbini mahali lilipopangwa pambano hilo kupigwa.


awali pambano hilo lilipangwa kuchezwa tarehe 29 mei lakini kamati ya mpito ya TPBRC ililisimamisha pambano hilo baada ya muandaaji wa pambano hilo Shomari Kimbau kutoka Golden Boys Promotion kushindwa kutimiza masharti na matakwa ya kimkataba, kukosekana kwa vibali vya pambano na kukosekana kwa vipimo vya afya kwa mabondia hao

Pambano hilo lilisogezwa mbele mpaka tarehe 31 na kupata vibali vyote na baadhi ya mapambano yalichezwa usiku huo lakini wasaa ulipowania kwa Mwakinyo na Partick Alotey kupanda ulingoni kuwania ubingwa wa WBO ndipo taarifa zikatangazwa kwamba pambano hilo halitafanyika kwani mwakilishi wa WBO hakufika uwanjani.

"Pambano kati ya Mtanzania, Hassan Mwakinyo dhidi ya Patrick Allotey la kuwania Ubingwa wa Afrika mkanda wa WBO halijafanyika kwasababu mwakilishi wa WBO Afrika, SAMIR CAPTAN hakufika ulingoni."

Hili linakuwa ni pambano la pili kwa mwakinyo kutochezwa na sababu mbalimbali ikiwamo bondia kulalamikia mikataba mibovu  kati ya bondia na promota aliyeandaa pambano hilo.


Post a Comment

0 Comments