BETI NASI UTAJIRIKE

REAL MADRID YAANDIKA HISTORIA MPYA UEFA

 Klabu ya Real Madrid imeendeleza ubabe wake katika michuano ya ligi ya mabingwa ulaya baada ya kuitandika Borussia Dortmund mabao 2-0.Ushindi huo umeipa Real Madrid taji lake la 15 tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo.

Real Madrid walikuwa wa kwanza kupata bao la uongozi kupitia kona iliyounganishwa kwa kichwa na Dani Carvajal dakika ya 74  na bao la pili liliwekwa kimiani na Vinicius Junior akimalizia pasi maridadi kutoka kwa Jude Bellingham dakika ya 83.

Tathmini ya Mchezo

Mchezo huo ulichezwa kiufundi mno kwa timu zote mbili hasa kipindi cha kwanza ambacho Dortmund walitengeneza nafasi nne za wazi lakini hawakupata bao lolote kutokana na umahili wa kipa Courtois. Baadhhi ya wachezaji wa Dortmund walionyesha umahili mkubwa ni Ryerson aliyefanikiwa kumdhibiti vinicious kipindi chote cha kwanza.Karim Adeyemi ni nyota mwingine wa Borrusia Dortmund aliyekuwa akiisumbua safu ya ulinzi ya Real Madrid na alifanikiwa kupata nafasi mbili ambazo zingezaa mabao.

kwa upande wa Real Madrid Carvajal alionyesha umahili wake kabla na baada ya kufunga bao, akiisaidia Real Madrid kupandisha mashambulizi kutokea pembeni na alifanikiwa kupata bao. Eduardo Camavinga ni jina ambalo hautaacha kulitaja katika mchezo huo kutokana na usahihi wa kila tukio la kiukabaji na kuanzisha mashambulizi akisaidiana na Toni Kroos na Valverde katika safu ya kiungo.

Eneo la ulinzi kwa Real Madrid lilikuwa imara sana hasa upande wa kushoto uliokuwa ukiongozwa na Ferland Mendy akisaidiana kwa karibu na Nacho pamoja na Rudiger hawa waliifanya Real Madrid kuwa imara nyakati zote. pongezi za kipekee zimwendeee golikipa Courtois aliyezuia nyavu zake kutikiswa baada ya kuzima mashuti manne yaliyopigwa na Dortmund.

 Tathmini kwa wachezaji

Kiungo Karim Adeyemi ameonyesha umahiri mkubwa hasa katika kupandisha na kuzima mashambulizi ya wapinzani wake.

Toni Kroos anaondoka uwanjani tukiwa bado tunamhitaji. mkongwe huyu katika mchezo huo alitoa msaada wa bao moja lililofungwa na Carvajal lakini pia  alipata nafasi mbili za faulo na mipila yote ililenga lango lakini kipa Kobel wa Dortmund aliiona na kuizuia isiingie nyavuni.

Tathmini kwa makocha 

Kocha Carlos Ancelloti amekuwa na msimu mzuri baada ya kuiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa La Liga na UEFA huku akitarajiwa kuiongoza klabu hiyo katika michuano ya Uefa Super Cup dhidi ya Atlanta mwanzoni mwa mwezi August na michuano ya Kombe la dunia mwezi Disemba. 

katika mchezo dhidi ya Dortmund Anceloti alitumia mfumo wa 4-3-3 uliomfanya kuwa na mabeki 4 ambao ni Nacho,Rudiger,Mendy na Carvajal huku eneo la kiungo likiundwa na Camavinga ,Kroos na Valverde na eneo la mwisho la ushambuliaji liliongozwa na Vinicius ,Rodrigo na Bellingham. 

mfumo huu umempa mafanikio makubwa kocha huyu baada ya kucheza michezo 13 ya Uefa na kushinda michozo 10 na sare 3 akiwa hajafungwa mchezo wowote. katika hatua ya makundi Real Madrid ilimaliza ikiwa na alama 18 katika michezo 6 waliyocheza.

Mfumo huu uliiisaidia Real Madrid kuwaondoa Rb Leipzig, Manchester City na Bayern Munich katika hatua mbalimbali.mwalimu Ancelloti amekuwa muumini wa mfumo huo tangu mwanzo wa taaluma yake.


Post a Comment

0 Comments