BETI NASI UTAJIRIKE

NEYMAR AMGALAGAZA TENA RONALDO

 Klabu ya Al Hilal ya nchini Saudi Arabia imeendeleza ubabe wake mbele ya Al Nassr baada ya kufanikiwa kuchukua kombe la Mfalme. Al Hilal iliibuka na ushindi wa penati 5-4 dhidi ya Al Nasr katika fainali iliyopigwa katika ndimba la King Abdulah Sports city stadium  jijini Jeddah.

Katika mchezo huo mshambuliaji Aleksandar Mitrovic alikuwa wa kwanza kupachika bao katika dakika ya 7 lakini Ayma Yahya akasawazisha bao hilo dakika ya 88 na kuzifanya timu hizo kumaliza  dakika 90 wakiwa na sare ya mabao 1-1. Mchezo huo ulitawaliwa na kadi nyekundu 3 kwa wachezaji Ali Abdulayhi dakika ya 87,Koulibary dakika ya 90( Al Hilal) na David Ospina dakika ya 57(Al Nassr).

Dakika  30 ziliongezwa lakini timu hizo hazikufungana na mwamuzi kuamulu mikwaju ya penati ambapo Al Hilal walipata penati zote 5 na Al Nassr walipata penati 4

Ushindi wa kombe la Mfalme unaifanya Al Hilal anayoichezea Neymar kufanikiwa kutwaa makombe mawili ndani ya msimu mmoja.Al Hilal walifanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu (Roshin Saudi Pro League ) kwa alama 96 katika michezo 34 wakifuatiwa na Al Nassr waliofanikiwa kukusanya alama 82 pekee.

Kwa upande wa tuzo Cristiano Ronaldo allibuka  mfungaji bora wa ligi baada ya kufunga mabao 35 akifuatiwa na Aleksand Mitrovic aliyefunga mabao 28. 

Riyadh Mahrez aliibuka mchezaji aliyetengeneza pasi nyingi za mabao akifanya hivyo mara 13 akifuatiwa na Reuben Neves pasi 12 na Cristiano Ronaldo mara 11.


Post a Comment

0 Comments