BETI NASI UTAJIRIKE

MBAPPE,RONALDO NA HARRY KANE WAPOTEZWA NA MADOGO EURO 2024

 Kabla ya Ufunguzi wa michuano ya Euro 2024 nchini Ujerumani majina ya Cristiano Ronaldo, Mbappe na ,Harry Kane yalikuwa yakiimbwa mno katika kinyang'anyilo cha mfungaji bora wa michuano hiyo. Criastiano Ronaldo alikuwa mfungaji bora wa ligi ya Saudi Arabia, Harry Kne alikuwa mfungaji bora wa Bundesliga na Mbappe alikuwa mfungaji bora wa ligi ya Ufaransa na wengi tulitegemea nyota hawa wangeonyesha cheche katika hatua hizi za awali lakini mambo yamebadilika na sasa si nyota hao tena wanaotajwa kugombea kiatu hicho cha dhahabu.

Majina ya vijana wadogo kama Jamal Musiala,Ivan Schraz,Kai Havert,Jude Bellingham,Fabian Luiz na wengine wengi= ndiyo yameshikilia chati 

Jamal Musiala mabao 2

Jamal Musiala amekuwa akiimbwa sana kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha katika mechi mbili za awali dhidi ya Scotland na Hungary. Nyota huyo alifanikiwa kufunga bao katika mchezo dhidi ya Scotland na kuisaidia Ujerumani kuibuka na ushindi wa mabao 5=1 katika mechi ya ufunguzi,nyota huyo aliisaidia tena timu yake ya taifa kwa kufunga bao moja kati ya mawili na kuiwezesha ujerumani kutinga hatua ya 16 bora ikiwa na alama 6 mabao 7 ya kufunga na kugungwa bao 1 pekee.

Ivan Schraz mabao 2

Ivan amegeuka shujaa wa taifa la Slovakia baada ya kufunga mabao 2 katika mechi mbili alizocheza mpaka sasa. Nyota huyu anayekipiga katika klabu ya Slavia Prague hakuwa na msimu mzuri katika ligi ya Czech First League baada ya kufunga mabao 2 na kutengeneza mengine manne. Uwezo wake katika michezo hii miwili umezua gumzo kutokana na kumudu nafasi mbalimbali ikiwemo Winga wa kulia,winga wa kushoto na mshambuliaji wa kati. kama Ivan ataendelea kufanya haya aliyoyafanya katika mechi za awali basi nafasi yake kama mfungaji bora inaweza kuwepo.

Nyota wengine walioanza vizuri na kufuinga bao 1 katika michuano hii ni Jude Bellingham,Kai Havert,Fabian Ruiz,Frolian Wirtz,Alvaro Morata,Bruno Fernandez,WoutPost a Comment

0 Comments