BETI NASI UTAJIRIKE

KELVIN JOHN AMFUATA ATHUMANI IDDI DENMARK

Nyota anayechipukia Kelvin Pius John (20) amejiunga na klabu ya Aalborg BK ya Denmark kwa mkataba wa miaka minne kutoka KRC Genk ya Ubelgiji.


Anakuwa Mtanzania wa pili kuchezea Aalborg BK baada ya Arhumani Iddi Machuppa aliyecheza kuanzia msimu wa 2007 hadi 2009 akıtumia jina la Mohamed Rajab.Akiwa Aalborg BK, Machuppa aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2008-2009 walipokuwa kundi moja na Manchester United ya England, Villarreal ya Hispania na Celtic ya Scotland.Man United na Villarreal zilisonga mbele huku Aalborg BK na Celtic zikitolewa.Kisoka,

 Kelvin aliibukia kituo cha Football House cha Mwanza mwaka 2015 kabla ya kuchukuliwa timu ya Vijana ya Taifa chini ya miaka 15, akapandishwa U17 na kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kabla ya

kuchukuliwa na akademi ya Brooke House College ya Harborough, Leicestershire, England.
Alicheza Brooke House College hadi mwaka 2021 alipochukuliwa na KRC Genk akianzia timu ya vijana U19 kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa mwaka 2022 ambako amecheza jumla ya mechi 42 na kufunga mabao manne.

Post a Comment

0 Comments