BETI NASI UTAJIRIKE

JIJI LA LONDON LAZIDI KUWAKA MOTO

 Mashabiki wa Real Madrid na Borusia Dortmund wamekwisha wasili jijini London Nchini Uingereza kuelekea fainali inayopigwa usiku wa leo katika dimba la Wembley. mashabiki hao wanaamini hao wanaamini hawataondoka mikono mitupu kutokana na ubora wa vikosi vyao.


Mara ya mwisho uwanja wa Wembley kuandaa fainali za Uefa ni 2013 kati ya bayern munich  dhidi ya Borrusia dortmund mchezo uliomalizika kwa Bayern Munich kutwaa kombe hilo kwa ushindi wa mabao 2-1. katika msimu wa 2018 timu za  Real Madrid na Borrusia Dortmund  zilikutana mara mbili hatua ya makundi na mchezo wa kwanza na wapili Real Madrid waliibuka na ushindi wa magoli 6-3 

 Historia

Real Madrid Madrid na Dortmund zimekutana mara 14 katika michuano ya Uefa na Real Madrid imeibuka na ushindi mara 6 na kufunga mabao 24 wakati Dortmund imeibuka na ushindi mara 3 na mabao ya kufunga 19 na sare 5. 

kuelekea mchezo huu wa fainali wachezaji Marcos Reus na Toni Kroos wataagwa rasmi na mashabiki wa soka baada ya kuvitumikia vilabu vyao kwa mafanikio ya kiwango cha juu. kwa upande wa Jude Bellingham yeye atakuwa na kila sababu ya kuonyesha ukubwa wake mbele ya mashabiki wa Dortmund ambao msimu wa 2022/23 alikuwa mchezaji wao tegemezi na sasa anakipiga Real Madrid.

safari ya vilabu hivi mpaka kufika fainali

Real Madrid 

Real Madrid ilipangwa kundi C na ikiwa na timu za Napoli,FC braga na Union Brlin katika kundi hili Madrid waliondoka na alama 18 wakishinda michezo yote. hatua ya 16 walikutana na RB Leipzig na walifanikiwa kuondoka na jumla ya mabao 2-1. hatua ya robo fainali walikutana na Manchester City na kufanikiwa kuibuka na mabao 4-3.Hatua ya nusu fainali walikutana na Bayern Munich na kufanikiwa kuibuka na jumla ya mabao 4-3 .

Dormund 

Dortmund walipangwa kundi F wakiwa na timu za PSG,New Castle na Ac Milan na walifanikiwa kuondoka na alama 11 wakishinda michezo 3 sare 2 na kupoteza mchezo 1 .hatua ya 16 bora walikutana na PSV na kuibuka na jumla ya mabao 3-1 ,hatua ya robo fainali walikutana na Atletico Madrid na kufanikiwa kupata matokeo ya 5-4.hatua ya nusu fainali PSG na kufanikiwa kushinda mabao 2-0 .

je mchezo huu una maana  gani kwa Borrusia Dormund

mara ya mwisho kwa Borrusia Dortmund kutwaa kombe la Uefa ni msimu wa 1996/97 na fainali ya mwisho kwa timu hiyo ni msimu wa 2013 waliopoteza kwa bayern munich katika dimba hili hili la wembley. wameingia tena hatua hii na mategemeo yao ni kutoondoka Wembley mikono mitupu.jambo la pili ni watamuagaje mkongwe marcos Reus aliyemwaga jasho na damu ndani ya klabu hiyo jibu ni jepesi tu Kombe hili litampa ushujaa na furaha ya kustaafu itazidi kuongezeka. swali ni je wataweza? binafsi naamini chochote kinawezekana ndani ya dakika 90.

Post a Comment

0 Comments