Lijendari Edson Cavani ametangaza rasmi kustaafu kuitumikia timu ya taifa Uruguay zikiwa zimesalia siku 13 pekee kuelekea michuano ya Copa America 2024 nchini Marekani. Nyota huyo mwenye miaka 37 ametangaza rasmi kuitumikia Uruguay akiwa na mabao 58 katika michezo 136.
Cavani alianza kuitumikia Uruguay mwaka 2008 na aliisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa Copa Amerika mwaka 2011. Cavani anakumbukwa zaidi mwaka 2010 baada ya kufunga mabao 5 kombe la dunia nchini Afrika Kusini na moja ya bao lake kuchaguliwa kama bao bora la mashindano.
Cavani hajaonekana uwanjani tangu mwaka 2022 baada ya Uruguay kutolewa hatua ya makundi kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar.
Nyota huyo amekuwa na mafanikio kwa klabu na timu yake ya taifa ambapo upande wa Klabu anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora namba mbili ndani ya PSG akifunga jumla ya mabao 138 katika mechi 200 na timu ya taifa anashikilia rekodi ya kuwa nafasi ya pili nyuma ya Luis Suarez akiwa na mabao 58. Cavani ametumikia vilabu mbalimbali ikiwamo Manchester United,PSG ,Napoli, Valencia na sasa yupo Boca Junior
0 Comments