BETI NASI UTAJIRIKE

CARLO ANCELLOTI HASHIKIKI NA REKODI ZAKE

 Kocha Carlo Anceloti amekuwa na msimu bora zaidi kuliko makocha wengi barani Ulaya baada ya kuisaidia klabu ya Real Madrid kutwaa kombe la ligi ya mabingwa Ulaya pasipo kupoteza mchezo wowote kwa msimu wa 2023/24

Ancelloti amekuwa na rekodi bora zaidi kwa msimu huu katika michuano hiyo baada ya kucheza michezo 13 na kushinda michezo 10 huku akipata sare katika michezo3 na kufanikiwa kutwa ubingwa wa Uefa .Kwa upande wa La Liga kocha huyo aliiongoza Real Madrid katika michezo 38 akifanikiwa kushinda michezo 29 sare 8 na alipoteza mchezo mmoja pekee.

Kwa ujumla kocha huyo ameiongoza real madrid katika  michezo 55 akipata ushindi michezo 42 sare 11 na amepoteza michezo miwili tu akiisaidia klabu yake ya Real Madrid kutwaa kombe la 15 la ligi ya mabingwa ulaya kombe la La Liga mara 33 na Super Copa kwa msimu huu

HISTORIA FUPI 

Carlo Anceloti alizaliwa tarehe 9 juni mwaka 1954 nchini italy.Julai 1 1975 alianza rasmi safari ya soka kama mchezaji na alijiunga na klabu ya Regiollo kisha U19 Parma,AC Parma,AS Roma na mwaka 1992 alistaafu soka kama mchezaji akiwa na kikosi cha Ac Milan

mwaka1992/93 alirejea katika soka kama kocha msaidizi wa kikosi cha Italy na ameendelea kuwa ndani ya fani hiyo akizitumikia klabu za Regianna,Juventus,Chelsea,Ac Milan,PSG,Bayern Munich,SSC Napoli,Everton Real Madrid kwa awamu mbili..

wadhifa wa Ancelotti

Kocha huyu anamiliki leseni ya juu kabisa ya ukufunzi (UEFA PRO LICENCE) akitumia mfumo wa 4-3-3 na amefanikiwa kutwaa jumla ya makombe 26 kama kocha . Kocha huyo anashikilia rekodi ya kutwaa makombe ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE mara 5 akitwaa makombe mawili akiwa na AC Milan na makombe 3 akiwa na Real Madrid na kumfanya kuwa kocha mwenye mafanikio zaidi kwa makocha wasiokuwa wastaafu.

kocha huyo amefanikiwa kutwaa kombe la dunia ngazi ya vilabu mara tatu akiwa na Real madrid mara 2 na Ac Milan mara moja.Makombe mengine ni UEFA SUPER CUP ,EPL,La Ligga,Serie A ,Bundesliga  na Ligue 1.

Hatma ya Anceloti

Kocha huyo ataiongoza Real Madrid mpaka mwaka 2026 kama mkataba wake unavyosema na mwaka 2024 ataiongoza klabu hiyo katika mashindano ya Uefa Super Cup,Supa Coppa,club world cup,la liga na Uefa champions league.

Kwa msimu wa 2025 kocha huyo ataiongoza Real Madrid katika michuano mipya ya kombe la dunia kwa vilabu itakayofanyika kwa mara ya kwanza nchini marekani.

Post a Comment

0 Comments