BETI NASI UTAJIRIKE

TEN HAG AREJESHA HESHIMA YA MANCHESTER UNITED

 Kocha Erik Ten Hag amefanikiwa kukiongoza kikosi cha Manchester United kutwaa kombe la FA kwa msimu wa  2023/24. hili linakuwa kombe la pili tangu kocha huyo alipojiunga na klabu hiyo mwaka 2022 akitokea Ajax.Kocha huyo amekiongoza kikosi hicho na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mabingwa wa ligi kuu  Manchester City.


Manchester United walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 30 kupitia Alejandro Garnacho Ferreira na dakika ya 39 kijana anayechipukia Kobbie maino aliandika bao la pili la mchezo huo. Manchester City walipata bao la kufutia machozi dakika ya 87 kupitia  Jeremy Doku

Manchester United imefanikiwa kutwaa kombe hili mara 13 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1871.Klabu ya  Arsenal wanaongoza kwa kutwaa kombe hilo mara 14. kocha Alex Ferguson amefanikiwa kuiongoza Manchester United kutwaa ubingwa huo mara 5 na kumfanya aingie katika vitabu vya historia ya michuano hiyo

Msimu wa 2022/23 Manchester City walifanikiwa kutwaa ubingwa wa FA kwa kuiadhibu Manchester United mabao 2-1 na msimu huu Manchester United wameibuka mabingwa wapya wa FA kwa idadi ileile ya mabao na kuufanya mchezo huo utafsiriwe kama kisasi.

Kocha Erik Ten Hag amekuwa na mafanikio tangu alipojiunga na mashetani hao wekundu kwani msimu wa 2022/23 aliiongoza klabu hiyo kutwaa kombe la carabao cup mbele ya Newcastle United kwa ushindi wa mabao 2-1 na hili likawa kombe la kwanza tangu mwaka 2017 pia alimaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi na kuifanya klabu hiyo ifuzu hatua ya makundi UEFA

Msimu wa 2023/24 haukuwa mzuri kwa klabu hiyo baada ya kumaliza ligi ikiwa nafasi ya 8 alama 60 na kudaiwa bao 1 (-1).lakini ubingwa wa FA umeirejesha manchester united kushiriki michuuano ya Europa league kwa msimu wa 2024/25 swali ni je mwendelezo huu wa kocha Ten Hag unaweza kuirejesha heshima ya klabu hiyo kwa siku za usoni?



Post a Comment

0 Comments