BETI NASI UTAJIRIKE

SIRI TATU ZA UBINGWA WA YANGA MSIMU WA 2023/24

 Klabu ya Yanga imefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara (NBC) Kwa mara ya 3 mfululizo na kuifanya klabu hiyo kufikisha idadi ya makombe 30 ya ligi tangu kuanzishwa kwake mwaka 1935. Yanga wamefaikiwa kutwaa ubingwa huo wakiwa na alama 77 katika michezo 29 waliyocheza huku nafasi ya pili ikishikiliwa na azam wenye alama 66 sawa na Simba.


Kwa msimu wa 2023/24 Yanga wamekuwa katika sayari nyingine ya soka letu. achana na ligi yetu hebu waangalie Yanga walioshiriki hatua ya makundi ligi ya mabingwa Afrika . Tazama jinsi walivyoleta ushindani mpaka kufika hatua ya robo fainali,tazama jinsi mbinu za mwalimu zilivyokuwa zikionekana kila alipobadili wachezaji uwanjani.na tazama namna wachezaji walivyojituma uwanjani na mwisho wewe mwenyewe utajisemea moyoni kwamba Yanga walistahili ubingwa huu wa ligi kuu.

sahau kuhusu ushindi wa mabao 5-1 walioupata dhidi ya mtani wao Simba au ile supu waliyokunywa pale jangwani mara baada ya kumchakaza mtani , hizi ni sababu zilizowafanya Yanga kutwaa ubingwa wa ligi kuu kiurahisi sana.

1.UIMARA WA WACHEZAJI

Yanga wametwaa ubingwa wakiwa wamefunga jumla ya mabao 67 wakifungwa mabao 13 pekee katika mechi 29. Golikipa Diara amekuwa mlinzi imara ndani ya kikosi hicho akisaidiana na koplo Ibrahim Bacca,Dickson Job,Nickson Kibabage,Yao Kwasi,Lomalisa na mwamnyeto hii ni safu imara zaidi ndani ya ligi yetu kwa msimu huu. wachezaji tajwa hapo juu wamekuwa wakibadilishana mara kwa mara lakini kombinesheni yao imekuwa haipotei na mara zote wamekuwa imara sana.

  Aziz Stephanie Ki anaongoza kwa idadi kubwa ya mabao akifunga jumla ya mabao 18. Aziz amekuwa akipata ushirikiano mzuri kutoka kwa wachezaji wenzake kama Clement Mzize,Mudathir ,Pacome ,Nzengeri na kuifanya safu ya ushambuliaji kuwa tishio. 

Eneo la katikati limekuwa likiongozwa na Harid Aucho .ubora wake,usahihi wa matukio na namna alivyokuwa anauamrisha mchezo ndiyo ulipelekea Yanga isigusike kabisa eneo hilo.Kila mchezaji aliyepata nafasi alionyesha umuhimu wake. wengi watakumbuka namna mkude alivyomiliki dimba la kati dhidi ya Mamelodi 

2.UBORA WA MWALIMU

Kocha Miguel Gamondi amekiongoza kikosi hicho vyema baada ya kupata ushindi katika mechi 25 akipata sare mechi 2 na kupoteza mechi 2 pekee.ikumbukwe kocha Gamondi alikabidhiwa mikoba ya kukinoa kikosi hicho mwanzoni mwa msimu na ameleta matokeo chanya ndani ya kikosi hicho.mfumo wake wa 4-3-3 ulikuwa na matokeo chanya kila wakati.baadhi ya wachezaji kama Denis Nkane ,Gift Fred ,Zawadi Mauya ,Kibwana shomari hawakupata nafasi za kucheza mara kwa mara si kwasababu hawana uwezo bali mwalimu alitakiwa kuchagua wachezaji wenye ubora zaidi yao kwa manufaa ya timu.

3. SAJILI BORA 

Sajili zilizofanywa na Injinia Hersi Said zimetoa majibu chanya na kuisaidia klabu hiyo kufikia malengo waliyojiwekea. Usajili wa wachezaji kama Max Nzengeri ,Pacome,Yao KWasi Atoura, Mkude pamoja na Guede umeonekana una manufaa ndani ya kikosi cha Yanga na kumfanya mwalimu Gamondi kuwa na chaguzi nyingi za wachezaji anaowahitaji katika mechi mbalimbali.

kana klabu ya Yanga itaongeza ufanisi wake zaidi ya hapa tutegemee kuwaona fainali ya ligi ya mabingwa kwa  msimu ujao 


Post a Comment

0 Comments