BETI NASI UTAJIRIKE

SHERIA ILIYOWATAFUNA YANGA IMEWAPA UBINGWA ZAMALEK

 Klabu ya Zamalek imefanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe la shirikisho kwa msimu wa 2023/24.hili linakuwa kombe la pili kwa klabu hiyo kutwaa tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo mwaka 2004. Zamalek walifanikiwa kutwaa kombe hilo baada ya kupata ushindi wa mabao 2-2 huku sheria ya bao la ugenini ikiwabeba.

Mchezo wa kwanza dhidi ya RS BERKANE ulipigwa nchini Morocco na RS BERKANE kuibuka na ushindi wa mabao 2-1. Mchezo wa pili umepigwa jijini Cairo Misri na Zamalek kuibuka kwa ushindi wa bao 1 lililofungwa na Ahmedi Amdi dakika ya 24.

Zamalek wamefanikiwa kutwaa ubingwa wapili baada ya kufanya hivyo mwaka 2018.Klabu hiyo inarekodi ya nzuri katika michuano ya CAF baada ya kufanikiwa kutwaa kombe la ligi ya mabingwa mara 5 ,Kombe la shirikosho mara 2 na kufanya kuwa na jumla ya makombe 7 ya Africa , kwa upande wa Ligi kuu nchini Misri ,Zamalek wamefanikiwa kutwaa makombe 14 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1911.

Yanga ndiyo klabu pekee kutoka ukanda wa Afrika Mashariki(CECAFA) Kufika hatuan ya fainali za kombe la Shirikisho Africa kwa msimu wa 2022/24 wakimenyana na USM ALGER mchezo uliomalizika kwa usawa wa mabao (2-2) na USM Alger wakitwaa ubingwa huo kwa bao la ugenini. Fiston Mayele akiibuka mfungaji bora 

Post a Comment

0 Comments