BETI NASI UTAJIRIKE

MANCHESTER CITY YAONDOKA NA TUZO TATU EPL

 Klabu ya Manchester City imefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza baada ya kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Westham na kufikisha jumloa ya alama 91 katika michezo 38 ya ligi hiyo.


Huu unakuwa ubingwa wa nne mfululizo kwa klabu hiyo na ubingwa wa 6 tangu Pep Guardiola ajiunge na kikosi hicho cha Manchester. Tangu kuanzishwa lwa mfumo mpya wa ligi kuu mwaka 1992 Manchester City imefanikiwa kutwaa ubingwa mara nane huku Manchester United ikiongoza kutwaa ubingwa huo mara 13.

Mbali na kutwaa ubingwa wa ligi kuu lakini pia Manchester City imefanikiwa kutwaa tuzo tatu zaidi ikiwemo Mfunngaji bora ambaye ni Erling Halaand aliyefunga mabao 27, kocha bora ni Pep Guardiola aliyeisaidia timu hiyo kutwaa Ubingwa huo na Phil Foden amechaguliwa kama  Mchezaji bora wa msimu. 

Phoden amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo baada ya kufunga mabao 19 akitoa msaada wa mabao 8 na kuisaidia Manchester City kutwaa ubingwa huo. kwa upande wa tuzo nyingine zimekwenda kwa David Raya golikipa Bora kutoka Arsenal, Mchezaji bora anayechipukia Cole Palmer kutoka Chelsea na playmaker ni Ollei watkin wa Aston Vila baada ya kutengeneza nafasi 13 za mabao.



Post a Comment

0 Comments