BETI NASI UTAJIRIKE

HUYU HAPA KOCHA MPYA WA LIVERPOOL

 Mara baada ya hapo jana aliyekuwa kocha wa Liverpool Jurgen Klopp kuaga rasmi,klabu ya Liverpool imetangaza mrithi wake ambaye ni Arne Slot aliyepewa mkataba wa miaka mitatu maka mwaka 2027 kukiwa na kipengere cha nyongeza kama atafikia malengo ya klabu hiyoJE ARNE SLOT NI NANI 

Arne Slot alizaliwa nchini uholanzi mwaka 1978.Mwaka 1995 alijiunga na klabu ya FC ZWOLLE kama kiungo na aliitumikia klabu hiyo katika michezo 164 na kufunga mabao 50. Mwaka 2013 alitangaza rasmi kustaafu  soka akiwa na jumla ya mabao 100 katika michezo 462 aliyocheza akiwa na vilabu vya fc zwolle ,pec zwole,Sparta AR, na nac breda zote za Uholanzi.

mwaka 2016 Arne Slot alirejea dimbani kama kocha na aliiongoza Cambuur kutoka mwaka 2016 hadi 2017 baadaye alihamia klabu ya AZ ambako alihudumu kama kocha mkuu kutoka mwaka 2019 hadi 2020. mwaka 2021 alijiunga na Feyenoyde mpaka mwaka 2024 mei 19.

KWANINI LIVERPOOL WAMKARIBISHE ANFIELD.

Uongozi wa Liverpool unaamini kocha huyo ni chaguo sahihi kwa mipango ya muda mrefu. rekodi ya msimu wa 2023/24 inaonyesha amecheza mechi 47 za mashindano yote na kufanikiwa kushinda michezo 32 sare 7 na kupoteza michezo 8 pekee.

mfumo wake wa kiuchezeshaji hauna tofauti na ule wa Jurgen Klopp (4-3-3) mabeki 4,viungo wa ushambuliaji 2 kiungo wa ulinzi 1 na washambuliaji watatu ambao Liverpool wamekuwa wakiucheza na kupata mafanikio makubwa lakini pia wanachagizwa na uwepo wa wachezaji wanaoendana na mfumo huo kama Mosalah,Nunez na Gakpo.

Uongozi wa liverpool unaamini kocha huyo atapunguza matumizi ya pesa za usajili kwa kuwaendeleza vijana wa academy na pia kusajili wachezaji wa gharama nafuu watakaomsaidia kuleta ushindani na  kutwaa makombe atakayoshiriki

itaendelea

Post a Comment

0 Comments