BETI NASI UTAJIRIKE

BAADA YA WAZEE DAY SASA NI GAMONDI DAY

 Klabu ya Yanga kupitia msemaji wake ALI KAMWE imejiandaa kumpa heshima ya kipekee kocha wa timu hiyo Miguel Gamondi. katika mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma mchezo utakaopigwa katika dimba la JAMHURI DODOMA .


Ali kamwe amenukuliwa akisema 

"Kocha Gamondi anastahili heshima ya kipekee kwa mambo makubwa aliyoyafanya msimu huu. kwanza ametupeleka robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika na pili ametuwezesha kutwaa ubingwa wa 30 wa ligi kuu hivyo basi ifikapo dakika ya 30 ya mchezo dhidi ya Dodoma  mashabiki wote watasimama na kumpigia makofi kama ishara ya kumheshimu"

Gamondi Day ni muendelezo wa klabu ya Yanga kutambua umuhimu wa kila mchezaji ,viongozi na hata mashabiki wao. Tunakumbuka namna wachezaji na mashabiki walivyochomekea siku ya max nzengeli,namna walivyobadili mitindo ya nywele kwa kupaka rangi siku ya Pacome day,uvaaji wa bukta siku ya azizi ki na namna walivyopiga simu siku ya mudathir yahya.

mbali na gamondii day klabu hiyo imepanga kusherehekea kubingwa wake wa ligi kuu tarehe 25 kutoka uwanja wa benjamini mkapa kuelekea makao makuu kwa ajili ya kujipatia supu kwa mashabiki na wachezaji wa timu hiyo na wameiita siku hiyo ni SUPU DAY.

Post a Comment

0 Comments