BETI NASI UTAJIRIKE

AL AHLY WAENDELEZA UBABE WAO LIGI YA MABINGWA

 Klabu ya Al Ahly imefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Esperance de Tunis.hili linakuwa ni kombe la pili mfululizo kwa klabu hiyo baada ya kulitwaa kombe hilo msimu wa 2022/23 .


Mchezo wa mzunguko wa kwanza kati ya Al Ahly na Esperance  ulipigwa nchini Tunisia na ulimalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu kwa sare ya bila kufungana(0-0) mchezo waraundi ya pili umefanyika nchini Misri na Al Ahly walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza  baada ya beki wa Esperance Roger Alohou kujifunga katika dakika ya 4 ya mchezo huo na mpaka refa anamaliza mchezo Al Ahly walikuwa mbele kwa bao 1-0 .

Matokeo hayo yanawafanya Al Ahly kufikisha idadi ya  makombe 12 ya ligi ya mabingwa Africa wakitwaa makombe hayo kuanzia mwaka 1982,1987,2001,2005,2006,2008,2012,2013,2020,2021,2023 na 2024. pia klabu hiyo imefanikiwa kufika fainali mara 17 na kushindwa kutwaa ubingwa mara 5.

Mpaka kufika hatua ya fainali Al ahly wamecheza jumla ya michezo 12 na hawakupoteza mchezo wowote na timu hiyo imefungwa bao 1 pekee na wamefunga jumla ya mabao 12 mpaka wanatwaa ubingwa wa michuano hiyo ,

Al Ahly wameondoka na kitita cha dola milion 4 kama zawadi ya bingwa wa michuano hiyo na Esperance wameondoka na kiasi cha dola milioni 2 kama zawadi ya mshindi wa pili. kwa upande wa wafungaji bora wamichuano hiyo Sankara karamoko kutoka Asec Mimosa anaongoza orodha ya ufungaji akiwa na mabao 4 katika mechi 3 na nafasi ya pili inashikiliwa na Pacome Zouzoua wa Yanga akiwa na mabao 3 katika mechi 5 alizocheza..

Al Ahly wanaongoza kutwaa ubingwa wa michuano hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1965 na wapinzani wao wa jadi zamalek wakishika nafasi ya pili kwa kutwaa kombe hilo mara 5 sawa na TP Mazembe ya DR CONGO.


Post a Comment

0 Comments