BETI NASI UTAJIRIKE

UFALME WA BENZEMA UNAVYOFUTWA NDANI YA MSIMU MMOJA

 Baada ya Karim Benzema kuondoka kisha kumkosa Harry Kane ni nani atakayeongoza safu ya ushambuliaji ya Real Madrid? Hili ni swali ambalo kila shabiki wa soka duniani alikuwa akijiuliza na kushindwa kupata majibu.

Wakati Benzema anatangaza kuondoka ndani ya Real Madrid viongozi wa klabu hiyo walitenga kias cha Euro milioni 100 ili waweze kumnasa Harry Kane lakini dili hilo lilishindikana baada ya nyota huyo kutua Bayern Munich.

Madrid waliamua kubadili uelekeo na kumsajili kwa mkopo mshambuliaji Jose Luis Mato maarufu kama Joselu kutoka Espanyol. Real Madrid walijikuta wakishawishika kumsajili mkongwe huyo kwani msimu wa 2022/23 nyota huyo alifanikiwa kufunga mabao 16 na kushika nafasi ya tatu ya ufungaji wa mabao nyuma ya Karim Benzema mabao 19 na Robert Lewandowski mabao 23.

Usajili wa Joselu kwa msimu huu ni kama hauna nguvu ya kuunda hoja kwani nyota huyo amecheza mechi 27 na kufunga mabao 8 pekee kwa michuano yote aliyoshiriki.

Mpaka sasa Madrid imeshacheza michezo 29 ya la liga ikijikusanyia pointi 72 na kufunga mabao 64 wakiongoza ligi. Kiungo mshambuliaji Jude Bellingham anaongoza kwa kufunga mabao mengi akifanya hivyo mara 16 . Msimu wa 2022/23 Karim Benzema alikuwa mfungaji namba mbili La Liga akifunga mabao 19 hivyo Bellingham anamechi 9 mkononi kuweza kufikia na kuvunja rekodi ya Karim Benzema kwa msimu uliopita.

Kwa sasa hauwezi kuwasikia mashabiki wa Real Madrid wakimuimba Benzema na yawezekana wameshauvua ufalme wake na kumpa Bellingham.

Post a Comment

0 Comments