BETI NASI UTAJIRIKE

HUYU NDIYE TISHIO KWA HALAAND NA MO SALAH MBIO ZA MVP 2023/24

 Kwa msimu wa 2023/24 klabu ya Aston Villa chini ya David Moyes imeonekana kuwa gumzo na tishio kwa kila mchezo wanaocheza. Moja ya jambo linalowapa gumzo mitandaoni ni uwezo mkubwa wanaouonyesha kwa msimu huu kwa kucheza michezo 29 wakishinda michezo 17 sare 5 na kufungwa michezo 7 wakiweka kibindoni pointi 53 na kushika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi nyuma  ya Manchester City Liverpool na Arsenal.

Yote yatasemwa kuanzia kwa kocha Unai Emery na ubora wake,udhamini wa makampuni makubwa kama Cazoo lakini kwangu ntagusa eneo moja tu ambalo ni safu mahili ya ushambuliaji inayoongozwa na muingereza Ollie Watkins.

Kwa msimu huu Aston Villa wamefunga mabao 60 katika michezo 29 waliyocheza sawa na wastani wa kufunga mabao mawili kwa kila mchezo wanaocheza. katika mabao hayo 60 Ollie watkins amefunga mabao 16 na kutengeneza mabao 10 hivyo kuwa na mchango wa mabao 26 kati ya yale 60

Mshambuliaji huyu anashika nafasi ya pili kwa ufungaji nyuma ya Erling Halaand mwenye mabao 18 na watkins ndiye kinara wa kupiga pasi za mwisho akifikisha assist 10 na kuongoza orodha ya waliotoa pasi nyingi za mabao.

JE WATKINS NI TISHIO KWA HALAAND NA MO SALAH

Hili ni swali ambalo majibu yake yatapatikana mwishoni mwa msimu lakini Halaand na Mo Salah wanatakiwa kupambana haswa kama wanahitaji tuzo hii ya thamani kubwa pale Uingereza.kama ligi ingemalizika kesho sina shaka kwamba Watkins angebeba tuzo hii

Post a Comment

0 Comments