VINICIUS JR AMPIGA BAO RONALDO REKODI YA EL CLASSICO

 Kiungo mshambuliaji Vinicius Jr usiku wa kuamkia leo ameisaidia klabu ya Real Madrid kutwaa ubingwa wa Supercopa espana kwa mara ya 13 tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo mwaka 1982


katika mchezo huo Vinicius Jr aliweka rekodi mbili kubwa . kwanza ni kufunga mabao matatu ndani ya kipindi kimoja akifanya hivyo dakika ya 7,10 na 39 na rekodi nyingine ni kuingia katika vitabu vya kumbukumbu kama mchezaji wa 7 kufunga hat trick kwa mchezo unaowakutanisha Barcelona dhidi ya Real Madrid.

Nyota waliowahi kufunga Hat trick katika El Classico ni Jesus Narro Sancho (Real Madrid), Ferenc Puskas (Real Madrid na huyu alifunga Hat trick mbili katika uwanja wa Santiago Bernabeu na Nou Camp). Ivan Zamorano (Real Madrid), Fernando Sanudo huyu alifunga mabao 4 dhidi ya Barcelona kwenye mchezo uliomalizika kwa Barcelona kufungwa mabao 8-2 

Garry Lineker (Barcelona), Mkongwe Romario (Barcelona) Ivan Zamorano( Barcelona)  ,Luis Suarez (Barcelona), Lionel Messi (Barcelona) Karim Benzema (Real Madrid na sasa ni vinicius Jr.

Hat trick hii inaongeza thamani kubwa kwa Vinicius Jr mbele ya mashabiki wa Real Madrid na wengi wanasema mfupa uliomshinda Cristiano Ronaldo kwa miaka 9 ndani ya Real Madrid basi umetafunwa na kijana wa miaka 4 tu ndani ya Real Madrid 


Post a Comment

0 Comments