Kikosi cha Cameroon kitaingia dimbani leo hii majira ya saa 2:00 kucheza mchezo wake wa mwisho kundi C dhidi ya Gambia mchezo unaotegemewa kuwa kivutio zaid kwa siku hii ya leo.
Kwanza ni namna ambavyo kundi limesimama.
Kundi hili linaongozwa na Senegal wenye pointi 6 baada ya kushinda michezo yake miwili ya awali dhidi ya Cameroon na Gambia.
Guinea wao wanapointi 4 wakishika nafasi ya pili baada ya kupata ushindi hizo dhidi ya Gambia na sare dhidi ya Cameroon
Cameroon anashikilia nafasi ya 3 akiwa na alama 1 aliyoipata dhidi ya Guinea. Na leo hii atavaana na Gambia ambaye hana alama yoyote.
Vita iko hivi
1.Ili Cameroon aweze kumaliza katika nafasi ya pili na kuingia hatua ya robo fainali anapaswa kupata ushindi wa mabao 3 dhidi ya Gambia na atafikisha pointi 4 akiwa na bao 1 la nyongeza
2.Ili Guinea aweze kumaliza nafasi ya kwanza atapaswa kumfunga Senegal ila kama atapata sare yoyote basi atamaliza nafasi ya pili hivyo kujihakikishia nafasi ya kwenda robo fainali .
3.Gambia ananafasi ya kumaliza nafasi ya 3 endapo atapata ushindi dhidi ya Cameroon na kufikisha point 3.nafasi hii itamfanya awe chaguo la kuingia mchujo wa kuingia robo fainali
Ni wakati wa Onana kurejesha heshima aliyoipoteza kwenye michuano hii.
Golikipa namba moja wa Manchester United na Cameroon amekuwa gumzo nchini mwaka na Dunia nzima imemgeuza mjadala
Kiwango chake akiwa ndani ya Manchester United kimekuwa gumzo kwa kuwa ameruhusu mabao mengi sana kwa msimu wake wa kwanza ndani ya kikosi hicho
Pili nyota huyo alichelewa kujiunga na timu yake ya taifa hivyo kuonekana hana nidhamu kwa taifa lake.
Tatu ni kiwango alichoonyesha kwenye mchezo dhidi ya Senegal mchezo uliomalizika kwa timu ya Cameroon kufungwa mabao matatu na yeye akiwa Langoni.Mengi yalizungumzwa na yanazidi kuzungumzwa.
Kocha Rigobert Song na benchi lake la ufundi wanamwamini nyota huyo. Mashabiki hawana imani na Onana .ni wakati sahihi kwa onana kuonyesha uwezo wake wote dhidi ya Gambia kurejesha matumaini kwa Wa Cameroon na mashabiki wa Manchester United ambao wanakerwa na ufanisi mdogo anaouonyesha akiitumikia timu yao
0 Comments