BETI NASI UTAJIRIKE

ONANA APIGWA BENCHI CAMEROON IKIFUZU ROBO FAINALI KIMAFIA

 Ni furaha iliyoje kwa taifa la Cameroon baada ya kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Gambia.

Cameroon walihitaji kupata ushindi katika mchezo huo huku wakiwaombea Guinea kupoteza mchezo wao dhidi ya Senegal na ndivyo dua zao zilivyoweza kujibiwa.

Mpaka dakika ya 86 Cameroon walikuwa nyuma kwa mabao 2-1.dakika ya 87 beki wa Gambia Gomez alifanya makosa yaliyopelekea kujifunga na kuwarejesha mchezoni .

Dakika ya 90+1 Christopher wooh alipokea pasi kutoka kwa Nkoudou na kufunga bao la tatu na kuifanya Cameroon kuibuka na mabao 3-2

Kwa upande wa Guinea wao wamepoteza mchezo kwa kufungwa mabao 2-0  dhidi ya Senegal na kuwafanya kumaliza hatua ya makundi wakiwa na pointi 4 sawa Cameroon lakini wametofautiana mabao ya kufunga .

Golikipa Andre Onana aliwekwa benchi katika mchezo huo na chanzo cha ndani kinaeleza nyota huyo amepishana na benchi la ufundi kwa kutotii maelekezo anayopewa mazoezin.

SENEGAL wamemaliza hatua ya makundi wakiwa na alama 9 

Huu hapa msimamo wa kundi CPost a Comment

0 Comments