BETI NASI UTAJIRIKE

MASWALI MATATU KWA MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED BAADA YA KUKALIA KUTIKAVU

 Manchester United imeendelea kuwanyima furaha mashabiki zake baada ya kushindwa kupata pointi tatu mbele ya Tottenham katika dimba la Nyumbani Old Trafford.

Mchezo wa Manchester United dhidi ya Tottenham Hotspurs ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2. Manchester United walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza likiwekwa kimiani na Rasmus Hojlund dakika ya 3,Huku Rashford akifunga bao katika dakika ya 40

Mabao ya Totenham yaliwekwa kimiani na  Richarson dakika ya 19 na bao la pili liliwekwa kimiani na Bentancur  dakika ya 46.

Kwa matokeo hayo Manchester United inasalia katika nafasi ya 7 ikiwa na alama 32 kwenye michezo 21 waliyocheza mpaka sasa. Kwa Upande wa Totenham wao wanasalia katika nafasi ya 5 wakiwa na alama 40 wakiziwinda nafasi 4 za juu.

Swali jepesi kwa Mashabiki wa Manchester United .Je timu yao inafeli wapi? nani aletwe kukomboa jahazi linalozama ? kwa mwendo huu dalili za ubingwa wa EPL na kushiriki Ligi ya mabingwa msimu wa 2024/25 wanaziona ?

Post a Comment

0 Comments