BETI NASI UTAJIRIKE

LAURATO MARTINEZ AIPA INTER MILAN KOMBE LA KWANZA 2024

 Hatimaye inter Milan wamefanikiwa kutwaa kombe lao la kwanza kwa msimu wa 2023/24 .inter walifanikiwa kutwaa kombe hilo baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Napoli mchezo uliopigwa nchini Saudi Arabia.



Laurato Martinez alifanikiwa kufunga bao hilo dakika ya 90+1 na kuifanya timu ya inter Milan kufikisha idadi ya makombe 8 ya michuano hiyo iliyoanzishwa mwaka 1988.

Mfumo wa michuano hii

Hapo awali super cup ilihusisha timu mbili tu ambazo ni ubingwa wa Serie A na bingwa wa Coppa Italy na kama ingetokea bingwa wa Serie A na bingwa wa Coppa Italy ni mmoja basi huchaguliwa timu iliyofika nafasi ya pili kwenye msimamo wa serie A

Kwa mwaka 2024 muundo wa mashindano hayo umebadilika na sasa unahusisha timu 4 ambazo zitacheza kwa njia ya mtoano na mshindi atakwenda fainali moja kwa moja.

Msimu huu timu zilizoingia katika mashindano hayo ni Fiorentina,Lazio,Inter milan na Napoli.

Michezo ya mtoano iliwakutanisha Fiorentina dhidi ya Intermilan na inter kupata ushindi wa mabao 3-0 

Mchezo mwingine ni Napoli dhidi ya Lazio mchezo uliomalizika kwa Napoli kushinda mabao 3-0.

Fainali hii ya 36 ilizikutanisha Napoli dhidi Inter Milan na Laurato Martinez ndiye aliyeibuka nyota wa mchezo kwa kufunga bao hilo muhimu.



Post a Comment

0 Comments