ZANZIBAR HEROES vs KILIMANJARO STARS ( 0,0) Bonge la Mechi..!! Bonge la Burudani..!!
Tathmini ya haraka haraka Vijana tumewaona ambamo kati yao kocha wa timu ya Taifa 🇹🇿
Adel Amrouche atajitwalia wachezaji 27 ambao wataingia kambini mara Moja Kwa ajili ya maandalizi ya AFCON 2024 Nchini Ivory Coast ✍️
Mjadala ni mkubwa kuhusu wachezaji wa Kimataifa, wengine wakisema ni wa kawaida baadhi wakijinasibu kuwa tumepata Mali..!!😎
Binafsi nina mtazamo tofauti kabisa, Mimi ninaamini Mpira ni Sayansi na Sayansi inaishi Katika Kanuni, wachezaji wetu wa Kimataifa wako na kitu ndio maana wako huko waliko na benchi la ufundi limewafuatilia Kwa kuzingatia ufundi na hatimaye kuwajumuisha Katika Kikosi Cha awali Cha jumla ya wachezaji 53 ambapo watachujwa kufikia 27 watakaoenda kambini Nchini Misri😎
Unamkumbuka @mnogsss aliyeitwa Kwa mara ya kwanza timu ya Taifa??? Alionekana kama hamna kitu, akaendelea kuitwa mara kadhaa mpaka sasa Kwangu Mimi ni first eleven wa timu ya Taifa 🇹🇿. Hawa wachezaji kutoka nje wengi wao huitaji muda zaidi wa kuzoena na kuzoea mazingira,tofauti na Novatus Dismas ambaye ameanzia Soka lake Azam FC akipita pia Biashara UTD kabla ya kwenda nje ya nchi,yeye anaonekana ameingia Moja Kwa Moja Kwa haraka zaidi ya wenzake.
Faida ya kuwa na wakina Ben Starkie ni kuwa wao wamepitia na wako Katika usimamizi Bora zaidi wa Mpira pamoja na mazingira Bora ,hivyo Kwa wao hatutegemei makosa Yale ambayo Kwa wachezaji wetu wa ndani huwa tunawatetea Kwa kuita makosa ya kibinadamu😎
Hata kama Adel Amrouche atawaacha baadhi Katika Kikosi chake Cha awali Cha AFCON,kuwaita TU Katika 53 wa mwanzo instosha Kwa wengine tukiweka akiba ya kuendelea kuwafuatilia na kuwaita Katika Majukumu mbalimbali ya timu ya Taifa kama friendly international ambapo huwa Kuna mechi nyingi sana Katika Mwaka
KAZI KWAKO ADEL AMROUCHE AFCON 2024🇹🇿⚽⚽⚽
0 Comments