BETI NASI UTAJIRIKE

MAKALA:SAFARI YA TAIFA STARS AFCON 2024 SEHEMU YA 1

 Zimesalia Siku 30 pekee Taifa Stars ielekee nchini Ivory Coast kushiriki michuano ya CAF-AFCON 2024. Mengi yanategemewa kutokea ndani ya siku hizi 30 huku maswali yakiulizwa je tumejiandaa kushiriki na kuleta ushindani ama tunashiriki kutaka kuonekana Tanzania imeshiriki michuano hii ya Afcon 2024? 

Maswali ya majibu haya yataanza kujibiwa katika mchezo wa kwanza kwa Taifa Stars dhidi ya Morocco mchezo utakaopigwa tarehe 17 January.

Mwalimu Abel Amrouchi anakibarua cha ziada kuhakikisha Tanzania inamaliza katika nafasi mbili za juu kisha kuingia hatua ya robo fainali, nusu fainali,fainali na mwisho wa siku tulete kombe la Africa nchini kwetu.

Kundi la taifa stars lina vigogo haswa wa mpira kihistoria. Timu kama Morocco ilifanikiwa kuingia hatua ya robo fainali Afcon msimu wa mashindano 2021.Zambia imekwishawahi kubeba taji hili la Afcon mwaka 2012 lakini pia DRC Congo wamekuwa na rekodi nzuri kwenye michuano baada ya kushiriki mara 9 na kubeba taji hili mwaka 1968 na 1974 huku wakimaliza nafasi ya tatu mwaka 2015 hii.

Tanzania tunaingia kwa mara ya tatu katika michuano hii baada ya kushiriki mwaka 1980 ,2019 na sasa 2024 huku mioyoni mwetu tukibeba matumaini ya kuandika historia mpya.

Mengi yanategemewa kutokea ndani ya siku 30 kabla ya mashindano haya na wengi wanatamani kuyajua na kuelewa sisi kama nchi tumejiandaaje?

Amospoti tumejiandaa kukuletea Makala mbali mbali zenye kuchambua timu yetu kuanzia maandalizi ya awali mpaka siku ya safari kuelekea ivory coast.

Mfuatiliaji wetu utapata nafasi ya kuwasikiliza wachambuzi nguli,walimu wa mpira na makapteni wa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu NBC.

Mitazamo ya viongozi wa TFF nao wamejipangaje kuhakikisha timu yetu inarejea nyumbani na kombe hili. Endelea kufatilia ukurasa huu upate uhondo kamili


Post a Comment

0 Comments