BETI NASI UTAJIRIKE

KWA SAJILI HIZI KOMBE LAZIMA LIENDE TANGA

 Klabu ya Coastal Union imejipanga haswa msimu wa 2023/24 na malengo yao ni kutwaa taji la ligi kuu au kombe la shirikisho (Asfc) au makombe yote watakayoshiriki msimu huu.

Kwanza wamefanya maboresho kwenye nafasi mbalimbali za utendaji ikiwemo kumleta afisa habari na msemaji wa klabu hiyo 

Pili kufanya maboresho katika benchi la ufundi kwa kumkabidhi mikoba kocha mzoefu Mwinyi Zahera kama mwalim mkuu wa klabu hiyo.

Tatu usajili wa wachezaji wenye historia nzuri na ligi yetu lakini pia wachezaji wa kigeni waliofanya vizuri katika ligi zao za nyumbani.

Mpaka sasa timu ya Coastal Union imecheza mechi 2 ikipoteza 1 na sare moja hiyo kuifanya akae nafasi ya 10 ikiwa na pointi 1 kwa sajili hizi tutegemee makubwa kwa raundi ya tatu dhidi ya Simba












Post a Comment

0 Comments