BETI NASI UTAJIRIKE

HATMA YA INONGA KUJULIKANA HIVI KARIBUNI

 Henock Inonga alipata maumivu ya mkono kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fountain Gate Uwanja wa Mkwakwani, Tanga dakika ya 89.


Nyota huyo hakuwa kwenye mchezo wa fainali dhidi ya watani zao wa jadi yanga

Inonga alikuwa shuhuda wa fainali hiyo iliyochezwa Agosti 13 Simba ikiwashinda watani zao wa jadi yanga kwa penalti.

Ally Salim alikuwa ni shujaa baada ya kuokoa penalti tatu za Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi aliyeanza kwa kasi ndani ya Ligi Kuu Bara.

Baada ya kuwa nje kwa muda amerejea mazoezini na wachezaji wenzake kwa maandalizi ya mechi zinazofuata ikiwa ni pamoja na mchezo dhidi ya Power Dynamo ya Zambia.

Huo utakuwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya pili na unatarajiwa kuchezwa Septemba 16,2023.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema wachezaji wote wanaendelea vizuri kwa ajili ya mechi zinazofuata.

“Inonga amerejea mazoezini akiwa pamoja na wachezaji wenzake hata Aubin Kramo naye pia yupo fiti kwa ajili ya mechi zinazofuata,”.

Post a Comment

0 Comments